Na.Wizara ya Madini - DSM
Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania itaendelea kuipa umuhimu pamoja na kushorikiana Wadau wa Maendeleo nchini katika kuendeleza mipango ya Taifa katika kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ndani ya Sekta ya Madini.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 26,2023 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipomwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar katika kufunga Mkutano wa tano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji wa mwaka 2023.
Mhe .Majaliwa amesema kuwa Serikali ipo tayari na inaruhusu miradi ya maendeleo kutoka Sekta binafsi katika Utafutaji , Uchimbaji , uchorongaji na uongezaji thamani madini ili kufanikisha mikakati iliyopo kwa wachimbaji kwa wachimbaji wote nchini.
Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa Serikali ina Taasisi yake ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambao wao wanafanya kazi ya utafiti , uchenjuaji na uchorongaji kwa kushirikiana na kampuni binafsi , hivyo wadau wote mlioshiriki mkutano huu tumieni fursa hiyo ya ushirikiano kimkakati.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali kupitia Taasisi ya GST ina mpango wa kufanya utafiti wa jiolojia kwa nchi nzima ifikapo mwaka 2030 ili kuwa na kanziData ya taarifa za jiolojia zitakazo tumika kuvutia wawekezaji wa madini ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake , Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde amesema wizara imetumia Mkutano huu katika kukuza ushirikiano wa kikazi baina ya nchi na nchi kupitia mada mbalimbali zilizowasilishwa kama vile majadiliano kuhusu matumizi ya Nishati safi ili kupambana na Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Mhe.Mavunde ameongeza kuwa sekta ya madini inaendelea kusimamia miradi mbalimbali nchini ambapo leo oktoba 26 , 2023 kampuni ya Noble Helium yaanza leo utafiti wa Gesi ya Helium mkoani Rukwa.
Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amesema kwa mwaka 2023 mchango wa wachimbaji katika sekta madini ilikusanya Shilingi Bilioni 678.
Awali , Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mathayo David Mathayo amesema kuwa kazi kubwa ya kamati ni kuishauri na kisimamia sekta ya madini ili ikamilishe malengo iliyojiwekea hivyo itaendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa Wizara na Taasisi zake.
Mkutano wa Madini na Uwekezaji Tanzania kwa mwaka 2023 ulibebwa na kauli mbiu inayosema "Bridging Tanzania Mining Sector to the World"
*VISION 2030* MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI.
Post A Comment: