Hifadhi ya Taifa Serengeti imeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Tuzo ya Hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2023(Africa’s Leading National Park 2023) ikiwa ni mara ya tano mfululizo kushinda Tuzo hii baada ya kuwagaragaza  washindani wa tuzo hii  kama Central Kalahari Game Reserve- Botwswana,  Etosha National Park -Namibia,  Kidepo Valley National Park -Uganda, Kruger National Park -South Africa, mapoja na Masai Mara National Reserve - Kenya

Tuzo hiyo imetolewa na ‘World Travel Awards’ usiku wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika hotel ya  _Atlantis The Royal Dubai  _ katika nchi za Falme za Kiarabu na kupokelewa  na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai, kwa niaba ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA).

Share To:

Post A Comment: