Na Ashrack Miraji
         (Same) kilimanjaro 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin babu amezindua jengo la Mama na mtoto katika kituo cha afya Bwambo Wilayani Same kinacho milikiwa na kanisa  katoriki jengo lililogharimu kiasi cha shilingi Milioni 450.

Akizindua jengo hilo  ambalo limejegwa  kwa ufadhili wa Shirika la partner for Hope lililopo Nchini Marekani  Mkuu huyo wa Mkoa Ameshukuru  kanisa katoriki kushirikiana na Serikali Katika kusogeza huduma kwa Wananchi.

"Kuwa na jengo hili la Mama na mtoto imekuwa msaada mkubwa kwa jamii hasa  akina Mama wanao jifungua watoto njiti, sisi kama Serikali hatuna budi kuwashukuru kwa  kuokoa maisha ya Mama na mtoto pia nawaomba wananchi wanufaika kuendelea kutumia huduma hii kwani ni sehemu ya uimalishaji wa huduma ya Afya kati ya kanisa na Serikali".alisema Nurdin Babu.

Kwa upande wake Askofu wa jimbo la Same Mkoani Kilimanjaro Mhashamu Rogath Kimario ametoa shukrani kwa Serikali kwa ushirikiano  kwenye nyanja mbalimbali  ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma muhimu, akishukuru pia viongozi wa kanisa kwa usimamizi mzuri kufanikisha Ujenzi wa jengo hilo ambalo limekua msaada kwa wakazi wa Same  wakiwemo waumini wa kanisa hilo kuwa na uhakika wa matibabu na huduma nyingine za kiafya.

Nae Mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni amesema kupatikana kwa mradi huo ni matokeo ya kuimatika kwa ushirikiano baina ya serikali na tasisi mbalimbali zikiwemo za binafsi   kutambua umuhimu wa kushiriki kuboresha upatikanaji wa huduma.

"Walicho kifanya wenzetu wa kanisa  katoriki ni Jambo la kushukuru na hii sio Mara ya kwanza kwan tumekua na ushirikiano mzuri  sisi kama serikali na wenzetu wa mashirika binasfi hakika wamefanya kazi kubwa pokeeni salamu za shukrani kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya Same".Alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya same.

"Kama serikali pia tunaendelea kutoa Rai kwa taasisi nyingine za Dini na ambazo siyo za Dini  kuunga mkono juhudi za serikali  chini ya Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassani kuleta Maendeleo chanya kwenye wilaya yetu na Taifa kwa ujumla".Alisema Mkuu huyo ya wilaya.




 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: