Na Mwandishi wetu Manyara.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Tanzania bara Komredi Mussa Mwakitinya (MNEC) amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzNia ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anamuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Jambarage Nyerere kwa Vitenda katika kupambana na Maadui matatu wa Taifa ambao ni Ujinga, Maradhi na Umaskini.
Komredi Mwakitinya ameyasema hayo tarehe 09 Oktoba 2023 alipowaongoza Viongozi na Wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kutembelea nyumba aliyofikia Baba wa katika harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika Mkoani Manayara.
Wakiwa katika Nyumba hiyo viongozi wa Jumuiya na Wachama walipata historia kutoka kwa mmoja wa wazee 13 ambao walitembea kutoka Manyara mpaka Dar es salaam kipindi cha kudai uhuru.
"Ndugu zangu Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan anamuenzi Baba wa Taifa kwa Vitendo katika kupambana na Maadau wa Tatu wa Taifa letu aliowaanisha Baba wa Taifa. Kwa Rais Samia anatoa Elimu Bila malipo awali hadi kidato cha Sita, na Chuoni anatoa mikopo ili watoto wote wapate Elimu.
Pili tumeona namna ambayo Rais wetu ameboresha Miondombinu ya afya, amejenga Zahanati, Vituo vya afya na hospitali kila mahali, Tatu tumeshuhudia mikakati mbalimbali ya kuboresha uchumi wa Watanzania hasa Vijana, kumeundwa baraza la uwezeshaji kitaifa lakini pia tunayo mikopo yetu ya Halmashauri kwa ajili ya Vijana na kina Mama. Huyu ndio Dkt Samia Suluhu Hassan"; Alisema Mwakitinya.
Aidha Ndugu Makitinya kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Vijana kujitokeza kwa wingi kuonyesha ni kiasi Gani wanamuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Samia Suluhu Hassan.
"Tupo kwenye Maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa, ambapo siku ya tarehe 14 Oktoba, 2023 ndio kilele cha Mbio za Mwenge na Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan ndio Mgeni Rasmi, niwasihi sana Vijana wenzangu tuje kwa wingi wetu tumuonyeshe Mama ni jinsi gani tunampenda na kumuunga mkono" Alisema Mwakitinya
Post A Comment: