Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein Mwinyi amezitaka nchi za Afrika kuheshimu utawala wa sheria na Utawala Bora ili kusaidia kulinda na kuimarisha haki za binadamu.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya haki za binadamu na watu Jijini Arusha ambapo amesisitiza nchi hizo kuendelea kuimarisha haki za binadamu na watu katika bara la Afrika.
Amesema ni Imani yake taarifa zitatoa tathmini ya hali halisi ya haki za binadamu na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kupata mbinu za kukabiliana na changamoto zitakazoainishwa katika Mkutano huu.
Aidha naamini kwamba washiriki watapata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusiana na masuala yatakayojitokeza katika taarifa zitakazo wasilishwa ambapo kikao hichi kitatanguliwa na majukwaa ya Taasisi za haki za binadamu zipatazo 46 na asasi za kiraia takribani 210 kutoka bara la Afrika.
"Tanzania inatekeleza na kusimamia haki za binadamu kwa Mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo ambapo haki za binadamu zimeanishwa kuanzia ibara ya 12 hadi 14 lakini pia Katiba yetu kuanzia ibara 25 hadi 30 imeainisha wajibu wa kila raia katika kuhakikisha tunalinda haki za binadamu na watu ndio maana tumeanzisha Tume ya haki za binadamu na Utawala Bora kwa lengo la kutetea kulinda na kuhifadhi haki za binadamu"
Vilivile hapa nchi serikali imechukuwa hatua kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na kutekeleza kwa mujibu wa mikataba ambayo Tanzania ni mwanachama kwa kiasi kikubwa jitihada zimeboreshwa ambapo Hali ya upatikanaji wa haki mbalimbali ikiwemo haki usawa mbele ya sheria Afya Elimu maji na Mazingira safi ,uhuru wa maoni, uhuru wa kuabudu ajira.
Hata hivyo kwa taarifa ni kwamba kutokana na uhuru huo hivi sasa Tanzania ina vyombo vya habari vingi vikiwemo redio 210 Television 56 na magazeti 288 pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Kwa mujibu wa Dkt.Mwinyi pia Tanzania imepiga hatua kubwa ya kuimarika kwa uhuru wa kidemokrasia, haki za wanawake Watoto na watu wenye ulemavu kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Post A Comment: