Na John Walter Babati
Mfuko wa pensheni Kwa watumishi wa umma (PSSSF), imeshiriki katika kutoa elimu juu ya huduma ya PSSSF kiganjani Kwa lengo la kurahisisha na kuwafikia wanachama pamoja na wastaafu kuweza kuwafikia huduma hiyo.
Hayo yamesema na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma PSSSF wakati wa maonyesho ya Biashara Katika Wiki ya Vijana Kitaifa, maadhimisho ambayo yanafanyika katika eneo la stendi ya zamani mjini Babati mkoani Manyara.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bwana Donald Maeda amesema katika Banda la PSSSF mwanachama atapata huduma zote za Mfuko zinazopatikana katika ofisi zote za Mfuko.
Huduma hizo ni pamoja na kupata taarifa za michango yake, kupata taarifa za mafao mbalimbali, Uhakiki wa Wastaafu pamoja na Elimu kwa Wanachama, pia Wanachama na Wastaafu wataunganishwa na huduma ya PSSSF Kiganjani.
Post A Comment: