Meneja Uhusiano kwa Umma PPRA, Bi. Zawadi Msalla, akitoa wasilisho la taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) 2022/23.

Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), imeokoa kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 2.6 ambazo zingepotea kupitia michakato ya ununuzi isiyozingatia sheria na taratibu, Meneja Uhusiano kwa Umma PPRA, Bi. Zawadi Msalla, amesema.

Ameyasema hayo mjini Morogoro wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) 2022/23, katika kongamano linaloshirikisha Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi zilizo chini Wizara ya Fedha mjini Morogoro,  Oktoba 25, 2023.

“Fedha hizo zimeokolewa baada ya Mamlaka kufanya ukaguzi katika taasisi 180, kupitia chunguzi maalum,” alifafanua.

Pia, PPRA ilifanya uchunguzi maalum kwenye taasisi 12 na kubaini kuwa Serikali ilipata hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 8.77 kwa kutozingatia sheria ya ununuzi, na kuishauri Serikali hatua za kuchukua dhidi ya wahusika ili kukomesha vitendo hivyo vinavyoligharimu Taifa, alisema Bi. Msalla

“Kuanzia mwakani PPRA itakuwa inawasilisha ripoti kwa Mheshimiwa Rais kama inavyofanya, Ofisi ya CAG na TAKUKURU,” Aliongeza.

Kuhusu Mfumo mpya wa Usimamizi wa Ununuzi wa Umma Kielektroni – NeST, Bi. Msalla alisema, mfumo huo umekamilika na ulianza kutumika rasmi Julai 1, 2023, na hivi sasa kwa mujibu wa maelekezo ya Mlipaji Mkuu wa Serikali kwa taasisi za umma, michakato yote ya ununuzi wa umma inafanyika kupitia Mfumo wa NeST pekee kuanzia Septemba 1, 2023.

Meneja Uhusiano kwa Umma PPRA, Bi. Zawadi Msalla, akitoa wasilisho la taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) 2022/23.
Bi. Msalla, akiwa na washiriki wengine, wakati wa kipindi cha majadiliano.
Baadhi ya washiriki 
Baadhi ya washiriki

Baadhi ya washiriki
Share To:

Post A Comment: