NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo, ameziagiza taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kutangaza utekelezaji wa majukumu yao ili umma wa watanzania ujue.

Bi. Omolo ameyasema hayo Oktoba 25, 2023, wakati akifungua Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi za Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari, mjini Morogoro.

“Taasisi zetu tumeziunganisha na masuala ya kiuchumi yanayohusu watu, nendeni mkajitangaze, mkijitangaza watu watajenga imani kwenu.” Amesema na kuongeza..Tumieni teknolojia katika kuwasiliana kwa sababu habari ni biashara na biashara ni fedha na fedha ni uchumi.” Amesisitiza Bi. Omolo.

Alisema, Mawasiliano ndio msingi wa mafanikio kwani kupitia, mawasiliano ndio wananchi wanapata fursa ya kujua shughuli zinazotekelezwa na taasisi hizo.

Aliwataka wakuu hao wa mawasiliano kuzijua vema taasisi zao na majukumu yanayotekelzwa na taasisi hizo.

Aidha amewaomba wahariri kupitia vyombo vyao, kuendelea kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya risiti za kielektroniki EFD, pindi wanapofanya manunuzi.

“Matumizi sahihi ya EFD yanaisaidia serikali kukusanya kodi ambayo ndio msingi mkuu katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.” Alifafanua.

Alitoa mfano wa miradi hiyo kuwa ni pamoja na ile ya kimkakati ya  ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, (JNHPP 2,115 megawatts), ujenzi wa reli ya kisasa SGR, na barabara za juu, (Fly overs).

“Hayo yote ni matokeo ya kulipa kodi na ndio maana tunasisitiza unapouza toa risiti halali na unaponunua dai risiti halali.” Alisisitiza

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Washiriki wa kongamano hilo, Bw. Ben Mwang’onda, ameishukuru Wizara ya Fedha, kwa kuridhia taasisi zilizo chini ya wizara kukutana na Wahariri, ili kueleza yale yanayotekelezwa na taasisi hizo.

“Jambo lolote ili lijulikane lazima litangazwe, hivyo hii ni changamoto kwetu sisi waandishi wa habari kwa fursa hii tuliyopewa ya kukutana na taasisi zilizo chini ya wizara, ili tujifunze yale wanayoyatekeleza na kisha tuwahabarishe wananchi.” Alisema Mwang’onda

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano hilo, Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano Srerikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, alisema, washiriki ni wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari na wakuu wa baadhi ya taasisi zilizo chini ya wizara ya Feha, Wizara ya Fedha ina jumla ya Taasisi 29.

“Huu ni muendelezo wa utekelezaji wa Mkakati wa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha, kukutana na wadau mbalimbali ili kueleza shughuli zinazotekelwa na serikali kjupitia Wizara ya Fedha pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara.

Taasisi 18 zinashiriki kwenye kongamano hilo la siku mbili.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo, akionyesha jarida linaloeleza taarifa mbalimbali za Uchumi wa Tanzania, wakati akifungua Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wa Taasisi za Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari, mjini Morogoro tarehe 25/10/2023.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo, akitoa hotuba ya ufunguzi.

Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano Srrikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akitoa neno la utangulizi.
Mwenyekiti wa Washiriki wa kongamano hilo, Bw. Ben Mwang’onda, akizungumzia utayari wa Wahariri katika kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji w amajukumu ya Wizara na Taasisi zake

Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi w akongamano hilo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo, akipena mikono na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, anayeshughulikia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Washiriki wa kongamano hilo, Bw. Ben Mwang’onda (kushoto) na Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi, Bw. John Samwel.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.

Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (kulia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, wakati wa Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka katika Taasisi zilizo chini ya Wizara na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, katika Ukumbi wa Mikutano wa 88 mkoani Morogoro Oktoba 25, 2023.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii.

Share To:

Post A Comment: