Kusuasua kwa Mkandarasi kuanza utekelezaji wa Mradi wa maji Kata ya Chimala wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya kumemlazimu Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kutoa maagizo ya mradi huo kuanza kutekelezwa jumatatu 30 Oktoba 2023 na ukamilike kwa wakati Ili Wananchi waweze kunufaika.
Licha ya mkandarasi huyo kudai kutokulipwa advance payment ndio sababu ya mradi huo kusuasua ,Mh Mahundi amelaani kauli hiyo inayotumiwa na wakandarasi wengi na kudai kipengele cha "Advance Payment" inabidi kiangaliwe upya maana wakandarasi wameona ndo kisingizio chao cha kuchelewesha kutekeleza miradi ya maji kwa wakati .
Viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya, kutokana na hali halisi ya ugumu wa upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama wemesikitishwa na kasi ndogo ya Mkandarasi inayosababisha mradi kuchelewa kuanza kwa wakati na wananchi kuendelea kuteseka kufuata maji umbali mrefu
Mradi huo unagharimu fedha kiasi cha shilingi Bilioni 4.5 ambapo utanufaisha wakazi wapatao 41,376 kwa vijiji 6 vya kata ya Chimala. Aidha, mkataba wa mradi huu ulisainiwa tarehe 01 Septemba 2023 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2024 hadi sasa utekelezaji wake ni asilimia 0.5
Post A Comment: