NAIBU Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Vijana Taifa Judith Kapinga amekabidhi gari lenye thamani ya milioni 18 kwa ajiri ya shughuli mbalimbali za Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (Uvccm) Mkoani Ruvuma


Akikabidhi gari hilo leo mbele ya Wajumbe wa Baraza la Vijana Mkoa kwenye viwanja vya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Ruvuma baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa Baraza Naibu Waziri Kapinga alisema kuwa gari hiyo iwe chachu ya kufanikisha shughuli za Jumuiya ya Vijana 

Kapinga alisema kuwa Vijana ni jeshi kubwa na ndio kiungo muhimu kwa uhai wa Chama na ushindi katika chaguzi za ndani ya chama na nje ya chama kwa kutambua hilo leo nakabidhi gari kwa ajiri ya Uvccm Mkoa, Kompyuta sita na Printa sita kwenye ofisi zote za Wilaya za Mkoa wa Ruvuma

Pia nakabidhi majiko ya gesi kwa kila Mjumbe wa Baraza la Vijana Mkoa, na kwa Viongozi wengine wa Chama ngazi ya Mkoa na Jumuiya zake, pamoja na watumishi wa Chama Mkoa wa Ruvuma

"Naamini Msaada huu mdogo ambao nimeutoa utakuwa chachu ya kuendelea kufanya kazi za Jumuiya na Chama kwa lengo la kuhakikisha ushindi unapatikana katika chaguzi ambazo zipo mbele yetu"Alisema Naibu Waziri Kapinga

Alisema kuwa Vijana tumeaminiwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hivyo tunawajibika kikamilifu kuchapa kazi kwa uweredi wa hali ya juu ili kuthamini Imani hiyo tuliyopewa na Rais

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Namtumbo George Luambano alisema kuwa tunampongeza Mbunge wa Vijana Taifa Judith Kapinga kwa kutukumbuka kutupatia vitendea kazi vya ofisi na kutupa majiko ya gesi

Luambano alisema kuwa msaada huo ambao ametupatia licha ya kuwa ni kumbukumbu muhimu kwenye vichwa vyetu lakini pia itaamsha hali mpya ya kuchapa kazi kwa nguvu zetu zote

Naye Mwenyekiti wa Uvccm Manispaa ya Songea Joachim Komba alisema kuwa kitendo cha Judith Kapinga cha kulikumbuka Baraza la Vijana Mkoa kwenye kila hatua ya maendeleo kinapaswa kuigwa na Viongozi wengine

Komba alisema kuwa licha ya Mbunge huyo kuwa na Majukumu mengi lakini amekuwa bega kwa bega na Vijana wa Mkoa wa Ruvuma kwenye kila hatua

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Ruvuma Kelvin Challe alimshukuru sana Mbunge Kapinga kwa kuithamini Jumuiya hiyo na kuahidi kusimamia kikamilifu vitendea kazi ambavyo wamekabidhiwa leo

Challe alisema kuwa gari ambalo wamekabidhiwa leo watalitunza kwa hali na mali ili liweze kufanya kazi kwa wakati wote kwani walikuwa wanahangaika sana kutekeleza Majukumu ya Jumuiya

Alisema kuwa majiko ya gesi ambayo wamepewa  licha ya kwenda kuwarahisishia shughuli zao za mapishi majumbani lakini majiko haya yanakwenda kuwa nishati rafiki majumbani mwao na hivyo kuendelea kulilinda taifa letu na matumizi ya nishati zinazozuiliwa kama kuni na mkaa ambazo matumizi yake yana athari hasi kwa Taifa letu.
Share To:

Post A Comment: