Mfumo wa ulipaji maji kwa njia ya kielektroniki katika  vyombo vya watumiaji maji(CBWSOs) utasaidia kuleta ufanisi wa utendaji kazi sambamba  na  ukusanyaji wa mapato katika vyombo hivyo.


Hayo yameelezwa na Kaim Meneja wa RUWASA Mkoa Mhandisi  Sospeter Lutonja wakati akifungua kikao kazi cha kuwaongezea uwezo watendaji  CBWSOs kutoka Wilaya saba za Mkoa wa Morogoro ambapo amesema mfumo wa MAJIIS utasaidia kuleta ufanisi wa kazi na ukusanyaji mapato kwenye vyombo vya watumiaji maji.


Amesisitiza  wateja kulipia huduma kulingana na miongozo ya serikali kutokana na  eneo husika   na sio baadhi ya watu kujipangia bei na kwamba lazima suala hilo kudhibitiwa.


Kwa upande wake mratibu na msimamizi wa uingizaji  wa huduma za watumiaji maji( CBWSOs) kwenye mfumo wa MAJIIS George Busunzu kutoka Wakala wa maji vijijini(RUWASA) makao makuu  na mratibu mfumo wa MAJIIS toka wizara ya Maji  mhandisi Masoud Almasi wamesema mfumo huo ulianza kufanya kazi kuanzia mwaka 2022 na unatekelezwa katika mamlaka  85 za Tanzania bara na moja Tanzania visiwani.

Mwisho





 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: