Afisa Mtendaji mkuu wa Mfuko wa utamaduni sanaa nchini Bi Nyakango Mahemba Taasisi ambayo ipo chini ya Wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo, iliyoanzishwa na Serikali kwa lengo la kuwainua wasanii ili kutengeneza kazi nzuri amewataka wasanii na waandaaji wa kazi za Sanaa hapa nchini kujitokeza ili kupewa mikopo itayoongeza ufanisi wa kazi zao.

Ametoa wito huo akiwa katika Wiki ya vijana kitaifa iliyofanyika mkoani Manyara Bi Nyakango amema Jumla ya Bil.3.5 zimetolewa na serikali Kupitia Mfuko huo tangu kuanzishwa kwake ambapo miradi 125 katika mikoa 12

Aidha Bi Nyakango amesema jumla ya ajira 59750 ambapo pia Mfuko wa utamaduni na Sanaa imesaidia katika uanzishwaji wa studio za kisasa 27 ambayo hutumika katika  kuzalisha kazi za sanaa na na kuwata vijana wajitokeze katika kutimiza ndoto zao kupitia Sanaa.

Bi Nyakango ameongezakuwa  ''ili mtu anufaike na mikopo yetu ni lazima awe Tanzania,awena umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, afanye kazi za utamaduni pamoja na Sanaa na vilevile anatakiwa ajisajili katika taasisi ya BASATA ambao wao ndiyo wapo kisheria katika kusimamia kazi za Sanaa pia Mwombaji anapaswa kuandika andiko la Miradi itayo elezea madhumuni na malengo ya mkopo wake''

Kwa upande wake Msanii wa Nyimbo za bongo Fleva Bw. Masinde Badi kutoka mkoa wa Manyara pamoja na wasanii waliofikiwa na kuelimishwa juu ya umuhimu wa mfuko wa utamaduni na sanaa, wameishukuru Serikali kwa kubuni na kuanzisha mfuko huo kwani utawasaidia wao katika kuongeza ufanisi na ubora wa kazi za sanaa hapa nchini jambo litakalokuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.



Share To:

Post A Comment: