Mkoa wa Mbeya umezindua zoezi la chanjo ya matone Polia kwa watoto waliochini ya umri wa miaka nane hafla iyofanyika kwenye Kata ya Iyela iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ajili ya kuwakinga na ugonjwa huo unaosababisha ulemavu wa kudumu na kupelekea kifo.
Akizungumza wakati wa kuzindua Chanjo hiyo ya matone ya Polio Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Juma Homera amesema kuanza kwa zoezi la chanjo kwenya mikoa Mbeya,Songwe,Katavi na Kagera kumetokana kuonekana kwa dalili za ugonjwa huo kwenye baadhi ya maeneo wamepatikana wagonjwa baada ya kuchukuliwa sampuli na kubainika watu hao wamepatwa na ugonjwa huo.
Homera ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan imeamua kuwakinga watoto na ugonjwa huo kwa maslahi mapana ya kizazi hiki na kijacho kwani bila kinga nchi itapoteza nguvu kazi ijayo na kujenga nchi itakayokuwa na wategemezi wengi kutokana na madhara ya ugonjwa wa polio ambao usababisha kupooza,ulemavu na kifo.
Mkuu wa Mkoa ametumia fursa hiyo kuwaeleza wazazi na walezi wasiwafiche ndani watoto wawatoe ama wawapeleke katika vituo vilivyotangazwa ili wapatiwe chanjo ya Polio waweze kuishi wakiwa na afya imara ili waje kuzijenga familia bora na nchi wakiwa na afya imara bila kushambuliwa au kupata madhara ya ugonjwa huo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mh.Dormohamed Issa ameishukuru serikali na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kwa kuamua zoezi la Chanjo ya polio lizinduliwe kwenye Jiji la Mbeya na ametua nafasi hiyo kuwaomba wakazi wa jiji la Mbeya kujitokeza vituoni na kwenye maeneo yaliyotangazwa kwa ajili ya kuwapatia Chanjo watoto waliochini ya umri wa miaka nane kwa kufanya hivyo ni kuwalinda watoto wetu na nchi yetu.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt.Yesaya Mwasubila amewasihi wananchi kuhakikisha wanafanikisha watoto wao waliochini ya umri wa miaka nane wanapatiwa chanjo ya polio na kubainisha kuwa chanjo hiyo ni salama haina madhara na haina usumbufu mkubwa wala mdogo kama ilivyokuwa kwa chanjo nyingine hasa za sindano.
Chanja ya Polio itatolewa kwenye Vituo vya Afya,Maeneo ya mikusanyiko kama masokoni,nyumba za ibada yaaani Makanisani,Misikitini,Shuleni na litafanyika zoezi la kupita nyumba kwa nyumba.
Post A Comment: