Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua tamasha la Mama Ntilie Festival Wilaya ya Rungwe Mkoani.

Jumla ya washiriki 136 wamejitokeza katika tamasha hilo ambapo wote wamepatiwa majiko na mitungi ya gesi na washindi 20 kila mmoja ametunukiwa mtaji wa shilingi elfu thelathini sanjari na kilo tano za mchele kila mmoja.

Mahundi amesema lengo la tamasha ni kuwawezesha wanawake kiuchumi bila kujali itikadi zao pamoja kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anawajali wananchi walio wanyonge.

Washindi 15 fedha zimetolewa na Mbunge wa Rungwe Anthon Mwantona ikiwa ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mhandisi Maryprisca Mahundi katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na kutunza mazingira.

Zoezi hilo litaendelea halmashauri ya Busokelo na washindi wa kwanza kila halmashauri watapatiwa mafunzo ya mapishi VETA ili kuboresha biashara zao.









Share To:

Post A Comment: