Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapa tabasamu wanafunzi zaidi ya 700 sekondari ya wasichana Kayuki iliyopo Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kwa kutoa msaada wa taulo za kike zaidi ya 1000 ambapo wanafunzi wa madarasa ya mitihani kidato cha nne na cha pili wao kila mmoja amepatiwa taulo mbili mbili ilhali kidato cha kwanza,tatu na tano wamepatiwa taulo moja moja.
Mahundi ametoa taulo hizo akiwa sekondari Kayuki akiwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne.
"Tumefundishwa mara nyingi kumtetea mtoto wa kike hasa katika hedhi salama hasa kidato cha nne kuelekea mtihani wa kidato cha nne"alisema Mahundi.
Mahundi ametumia fursa hiyo pia kueleza dhima ya kuanzisha taasisi yake ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) lengo likiwa ni kusaidia watoto na wanawake kiuchumi kauli mbiu yake Tukue Twende Pamoja.
Post A Comment: