Shehena ya  Bangi ikihusisha magunia 237 na kilo 310 za mbegu  imeteketezwa kwa moto kufuatia operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) kwa  kushirikiana na vyombo vya Ulinzi Usalama katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha .

Operesheni hiyo imesimamiwa na Mamlaka hiyo Kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Ni katika operesheni ya kupambana na kilimo na biashara haramu ya  Bangi kilichoshamiri eneo la Kisimiri  wilaya ya Arumeru ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Emmanuela Kaganda amesema lengo ni kubadilisha mtazamo wa wananchi katika kilimo na biashara ya Bangi

Innocent Masangulla ni Mkuu wa Operesheni wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa Mikoa ya Kanda ya kaskazini amesema Operesheni hiyo ni  ya tatu kufanyika Arumeru

Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Arumeru wamesema ni vyema serikali ikaongeza nguvu ya Kupambana na kilimo na biashara ya bangi Arumeru






Share To:

ASHRACK

Post A Comment: