Kasi ya maendeleo ya teknolojia lazima yamguse mwanamke kutokana na wanawake hasa wa vijijini kwani nao wana mchango mkubwa katika maendeleo ya teknolojia kwa maeneo mbalimbali ikiwemo kupitia simu za kijangani.
Akizungumza jijini Arusha kuzungumzia wiki ya Azaki inayoanza Oktoba 23 hadi 27 mwaka huu, ,Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki za Azaki, Nesia Mahenge amesema katika kasi ya maendeleo ya teknolojia nchini lazima yamguse mwanamke, ambaye ndiye mzalishaji wa kila kitu ikiwemo kilimo.
Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni Teknolojia na Jamii, ambapo wataangalia katika masuala ya teknolojia wapi walipotoka na wanapokwenda.
Amesema malengo ya mkutano huo ni kuimarisha uhusiano kati ya serikali na sekta binafsi, ikiwemo kuweka mikakati ya Azaki katika kutekeleza miradi kupitia teknolojia.
“Hivi sasa teknolojia inakua kwa kasi ikiwemo mabadiliko ya kidigitali, ambayo yana uwezo wa kuleta maendeleo mengi zaidi jumuishi,” amesema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk,Anna Henga amesisitiza wadau hao watajadili masuala ya sheria ikiwemo haki ya kumlinda mwanamke katika kujikwamua kiuchumi.
Post A Comment: