Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa mafunzo maalumu ya kudhibiti madawa ya kulevya kwa wanafunzi  1,141 na walimu 45 kutoka katika shule ya sekondari ya Kisimiri Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Elimu hiyo imetolewa baada ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini kufanya oparesheni katika kijiji cha Kisimiri na kukamata magunia ya bangi 237 na mbegu 310 yaliyoteketezwa juzi wilayani Arumeru.

Mafunzo hayo yametolewa na mamlaka hiyo kwakushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Arumeru Dorin Muhanika na Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini, Sara Ndaba walisema elimu hiyo itakuwa chachu kwa wanafunzi, walimu na wanakijiji wanaoishi eneo hilo kushiriki katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Muhanika amewataka wanafunzi wa shule hiyo kutokujihisisha na rushwa ya ngono pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi kwa kuwa vina madhara mengi ikiwemo magonjwa ya kuambukiza.

Huku Ofisa Ustawi wa Jamii ,Sarah Ndaba ametoa rai kwa wanafunzi hao kutokutumia madawa ya kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwaondoa kwenye fikra za rushwa na matumizi ya madawa hayo ya kulevya.

“Kunamadhara mengi ukitumia madawa unaweza kupoteza uwezo wa kufanya kazi ,kutokupata usingizi kudharaulika katika jamii vifo ,kufukuzwa shule kufeli mitihani na hata kufungwa kifungo cha maisha jela”

Angel Mlay ni moja kati ya wanafunzi wa shule hiyo ambapo amesema watakuwa mabalozi na kuwaelimisha wazazi wao ndugu ,jamaa na marafiki kuwa endapo watakamatwa wakijihusisha na kilimo,uuzaji au matumizi ya dawa hizo za kulevya watafungwa jela miaka 30 au kifungo cha maisha jela.



Share To:

Post A Comment: