Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema atakamilisha ujenzi wa nyumba ya mjane ambaye mume wake amepigwa risasi na mlinzi wa Kanisa la Katoliki halmashauri ya Wilaya Siha Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Mollel ametoa kauli hiyo leo katika mazishi ya mmoja wa wananchi wake aliyefariki Oktoba Mosi 2023 kwa kupigwa risasi na mlinzi wa kanisa hilo lililopo katika halmashauri hiyo Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Mollel ametoa kiasi cha Shilingi Milion 3 kama mwanzo, ikiwa ni mchakato na juhudi za kuanzia kazi ya ujenzi wa nyumba hiyo mara moja.
Aidha ametoa pole na faraja kwa wafiwa, masista wa Kanisa la Katoliki na wananchi wote kwa ujumla walioguswa na msiba huo na kuwataka kuendelea kuwa watulivu katika kipindi cha msiba.
“Ni mshukuru sista Mkuu wa Kanisa la katoliki Wilaya ya Siha kwa ushirikiano walioonyesha katika kukabiliana na msiba huu ni ishara tosha ya kuendeleza umoja na ushirikiano kati yao na wananchi”, ameeleza Dkt. Mollel
Katika hatua nyingine amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Siha pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa kuendelea kuhakikisha Siha inakuwa na amani na utulivu wakati wote.
Post A Comment: