Na Ashrack Miraji (Same)
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa shule mpya za sekondari kwenye kata tatu za Ndungu, Maore na Kisima kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kuwezesha wanafunzi walengwa kutumia majengo hayo kama ilivyo kusudiwa.
Ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake kwenye kata hizo mbili kujionea maendeleo ya ujenzi wa shule hizo mpya, zinazotekelezwa na serikali kupitia fedha za mfuko wa SEQUIP.
Katika ziara hiyo mkuu huyo wa wilaya ameshukuru uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye wilaya ya Same ikiwemo hiyo ya uboreshaji wa miundombinu kwenye sekta ya Elimu.
“Niwatake wakandarasi mlioaminiwa na serikali na kupewa kazi hii ya ujenzi, kuhakikisha mnakamilisha kazi hii kwa wakati kwa kuzingatia mikataba lakini pia lazima ujenzi kuwa katika ubora na viwango vinavyo kubalika kwakua mara kwa mara nitakuwa nikipita na kamati yangu kujiridhisha tunataka kuona thamani ya fedha iendane na ubora wa mradi”.Alisema mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha amemtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wataalam wake wanafata taratibu zote wakati wa manunuzi na kufuatilia kwa karibu kuepuka mianya ya Rushwa na utendaji mbovu na kutia dosari miradi hiyo pia kutekeleza ushauri na maelekezo yanayotolewa na vyombo vya usalama kwenye utekelezaji wa miradi.
Amewataka pia Halmashauri kuchukua hatua za haraka kutafutia ufumbuzi majengo ya shule ya Msingi Mtundu ambaysehemu kubwa ya kuta zake zina nyufa nyingi hali ambayo inahatarisha usalama wa wanafunzi wanaotumia majengo hayo.
Wakati huohuo mkuu huyo wa wilaya ameagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi kujiridhisha na mchakat mzima wa upatikanaji wa wakandarasi wanaopewa kazi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali wilayani huyo, na kuchukua hatua stahiki wanapobaini mapungufu ikiwemo ukiukwaji wa sheria.
Post A Comment: