Na Ashrack Miraji (Same) kilimanjaro
Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amemtaka mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Same Anastazia Tutuba kuangalia uwezekano wa kuzungushia uzio eneo kulipojengwa Hospitali mpya ya wilaya kuimarisha ulinzi wa vifaa na lasirimali muhimu zilizokwisha pelekwa katika eneo hilo akisisitiza pia usimamia wa karibu kukamilisha maeneo yaliyobaki.
Ametoa maagizo hayo wakati wa mwendelezo wa ziara zake alipotembelea hospitali hiyo kujionea maendeleo ya utekelezaji wake, ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza kuridhishwa na hatua iliyo fikiwa ikiwemo ubora wa Mejengo ikizingatiwa tayari huduma zimeanza kutolewa kwa wagonjwa wa nje.
Mradi huo ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Same uliibuliwa kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo kutokana na hospitali inayotumisa sasa kukabiliwa na uchakavu, kuelemewa kutokana na ufinyu wa eneo lenyewe ukilinganisha na idadi ya watu pia ni utekelezaji wa ahadi ya Rais kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.
Mradi huo hadi kukamilika kwake umepangwa kugharimu kiasi cha shilingi Bilioni saba, awamu ya kwanza ni ujenzi wa Majengo matano Jengo la wagonjwa wa nje, Stoo ya Dawa, Jengo la maabara, jengo la vipimo vya Mionzi na jengo la Wodi ya wazazi na Upasuaji na awamu ya pili ikihusisha umaliziaji wa majengo ya awali na uendelezaji wa majengo matatu,Utawala, jengo lakufulia na kichomea taka na shimo la kutupia majivu ambapo imepangwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2023.
“Tuweke wazi changamoto zote ambazo zinaweza kusababisha mradi kushindwa kukamilika kwa wakati ili tuweke msukumo wa pamoja, tukiendelea na ushirikiano huu ninauhakika hakuna kitakacho tukwamisha, tusiishi kama kisiwa sisi viongozi kwa umoja wetu kila mmoja ananafasi ya msukumo kwa nafasi yake”.Alisema mkuu huyo wa wilaya.
Amesema kukamilika kwa mradi huo mkubwa kutawezesha wakazi wa wilaya ya Same na maeneo jiani kuwa na uhakika wa matibabu ambapo mpaka sasa Zaidi ya shilingi Bilioni 2.06 zimetumika kwenye utekelezaji wa mradi huo, ikijumuisha kiasi cha shilingi Bilioni 2 fedha zilizotolewa na serikali kuu na kiasi kilich baki ni mchango wa wananchi kujitolea eneo la ujenzi ambao mpaka sasa umefikia asilimia 99.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mganga mkuu wa wilaya ya Same Dkt.Alex Alexander hospitali hiyo imekwisha sajiliwa tayari kutoa huduma ikizingatiwa wamekwisha pokea asimilia kubwa ya vifaa muhimu ikiwemo Dawa na vifaa tiba.
“Hospitali imesha sajiliwa kwa hadhi ya Hospitali ya Wilaya na Ile hospitali yetu Kongwe ambayo inatoa huduma tumeibadilisha jina na sasa inaitwa Same Town Hospita, Pia tumepokea na kusimika vifaa tiba mbalimbali kutoka MSD na vingine kutka Hospitali yetu ya wilaya kwa ajili ya kuanza kutoa huduma”.Alisema mganga mkuu.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amefanya mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero mbalimbali katika Kijiji cha Mwembe ambapo changamoto kubwa ni viongozi wa vijiji kutuhumiwa kuuza ardhi liyotengwa kwa ajili ya mifugo ambapo ameagiza ardhi hiyo kurejeshwe kwenye serikali ya kijiji kwakuwa taratibu za utwaaji wa ardhi hazikuzingatiwa pia viongozi waliohusika kuuza ardhi hiyo kurejeshe fedha kwa wahusika
Changamoto nyingine ni wafugaji kuvamia maeneo ya wakulima na kuharibu mazao ya wakulima ambapo nimeagiza mifugo inayoingia ikamatwe na kupigwa faini kwa mujibu wa sheria za mifugo ili iwe fundisho kukomesha tabia hiyo.
Mwisho.
Post A Comment: