Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe.Farida Mgomi amewaagiza viongozi wa serikali wilayani humo kutoa ushirikiano na machifu kukemea matukio ya uvunjifu wa amani na uharibifu wa mazingira.


Mhe.Mgomi amesema hayo Oktoba 2,2023 wakati akizungunza na wananchi,viongozi wa serikali na baadhi ya machifu katika Kijiji cha Ikimbilo lata ya chitete ikiwa ni siku maalumu ya kudumisha utamaduni.

Mhe.Mgomi amesema viongozi wa serikali ngazi ya Kijiji,kata na tarafa kuacha tabia ya kudharau jitihada za machifu wanapokemea uharibifu wa vyanzo vya maji, mazingira na maovu yanayohatarisha amani ikiwepo ubakaji na ulawiti Kwa watoto.

"Kama chifu anaona uharibifu wa mazingira wanakemea alafu viongozi wa serikali mnachekelea tuache mara Moja kuanzia Sasa kwani kiongozi wa Mila na viongozi wa serikali tunajenga nyumba moja" amesema Mhe.Mgomi.

Mhe.Mgomi amewataka pia viongozi wa serikali na Mila kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka pamoja na sheria bila kudharaulina na kuingiliana majukumu ya Kila mmoja.

"Sote tunatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria kanuni za taratibu za nchi yetu zilizopo kwenye katiba ili lengo letu litimie kiutamadumi", amesema Mhe.Mgomi.



 
Share To:

Post A Comment: