Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM,Wilaya ya Geita imeelekeza kuangezwa kasi ya usambazaji wa mbolea ya ruzuku kwa wakulima inayotolewa na serikali kwa lengo la kusaidia wakulima waweze kupata kwa wakati katika msimu huu wa kilimo ambao umekwisha kuanza.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Geita,Barnabas Mapande wakati akisoma maazimio matatu ya mkutano huo ambao umeketi kujadili taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya kuanzia January hadi Juni Mwaka Huu.amesema ni vyema usambazaji wa mbolea ukaendana na msimu wa kilimo.
“Msimu wa Kilimo umeanza Kupitia kikao cha halmashauri kuu tunaomba serikali ya wilaya iongeze kasi ya kuwasambazia mbolea wakulima wetu ,Serikali imetoa mbolea ya Ruzuku kwa lengo la kuwasaidia wakulima kulima kilimo ambacho kitakuwa na tija hatutaki kuona wanakuja na malalamiko ya kukosekana mbolea kwa wakati”Barnabas Mapande Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita.
Naye Katibu wa siasa na uenezi wa CCM Wilaya ya Geita,Gabriel Nyasilu amesisitiza kwa serikali ya Wilaya hiyo kuongeza msukumo wa usambazaji wa Mbolea kwa kuhakikisha zinawafikia kwa wakati wakulima huku akitoa onyo kwa baadhi ya mawakala ambao wanasambaza kuacha tabia ya kuwazungusha Wakulima.
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Cornel Magembe amesema wapo tayari kutekeleza maagizo ya Halmashauri kuu ya chama kwani nia yao ni kuona sasa wakulima wanafaidika na shughuli za kilimo ambazo wamekuwa wakizifanya kwa lengo la kutoa matokeo chanya ambayo yanaendana sambamba na kasi ya Mhe,Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwasaidia na kuwanyanyua wakulima.
Katika Kiko hicho cha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Geita,Imepokea taarifa mbali mbali za utekelezaji wa Ilani ya Chama zikiwemo za taasisi za serikali .TANESCO,MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA GEUWASA,TRA NA WAKARA WA HUDUMA YA MISTU TFS.
MWISHO…
Post A Comment: