Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni 4 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Siha kujenga shule ya wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa  Jimbo la Siha,  ambaye  pia  ni Naibu  Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake katika jimbo la Siha ambapo amepata kutembelea vijiji vitatu vya Magadi, Wiri na Mawasiliano na kujionea maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika vijiji hivyo

Dkt. Mollel amewaeleza wananchi wa vijiji hivyo kuwa shule hiyo ya wasichana itakapo kamilika itatatua changamoto ya watoto wakike kutomaliza masomo yao kwani wataweza kusoma kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha tano

Amesema kuwa Rais Dkt. Samhia Suluhu Hassan amewekeza sana katika jimbo Siha kwa kuhakiksha kila kijiji kinapata shule za kutosha ili kuepuka watoto kutembea mwendo mrefu kufata elimu.

“ Rais Samia amekua kiongozi wa mfano kwani ni mtu wa matokeo na leo wapiga kura wangu mumeona shule zilivyo jengwa na katika shule hii ya wasichana itajengwa shule ya ghorofa na tayari ujenzi umeanza”, Ameeleza Dkt. Mollel

Aidha amesema kuwa Serikali ya Dkt. Samia pia imetoa kiasi cha Shillingi Bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha veta katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha .

“Hivyo ni jukumu letu kama wazazi na walezi kuhakikisha vijana wetu wanapata ujuzi wa taaluma mbalimbali katika chuo hicho kipindi kitakapo kamilika na hivi sasa ujenzi unaendelea”, ametoa wito Dkt. Mollel

Lakini pia amesema kijiji cha Wiri asilimia kubwa ya watu tayari wana umeme na watu 30 waliobaki wataunganishiwa hivi karibuni na kufanya kijiji chote kuwa na umeme

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amesema kuwa wanampango wa kujenga shule ya watoto yatima katika wilaya ya Siha ambapo shule hiyo itagharimu kiasi cha Bilion  6.

Vile vile amesema kuwa wanasambaza matanki ya kuhifadhi maji  ya lita 10  kwenye  shule zenye  ukame  zaidi ili kusaidia kuhifadhi maji pale yatakapo kuwa hayapatikani 

Mbunge huyo amesikiliza changamoto ya wakina mama wajasiliamali katika Wilaya hiyo walio omba bati 30 kuezeka eneo wanako fanyia biashara zao na mbunge amesema kutoa bati hizo ili wakina mama hao kufanya shughuli zao katika mazingira rafiki na wao.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Magadi, Bi. Magret  Paul  amemshukuru Mhe. Mbunge kwa kutatua changamoto ya wakina mama kwa kuwapatia bati 30 ili kuezeka eneo wanalofanyia biasha zao








Share To:

Post A Comment: