Mbunge wa viti maalum CCM Mkoa wa Pwani na mjumbe wa kamati ya utekelezaji UWT Taifa Mhe. Subira Mgalu amewataka wananchi wa wilaya ya Biharamulo na Tanzania kwa ujumla kutokubali upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu juu ya mkataba wa DP WORLD.
Mgalu ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Nyakanazi wilayani Biharamulo kwenye mkutano wa hadhara ambapo amesema kuwa wale wote wanaopiga kelele juu ya mkataba wa Bandari wanapambania maslahi yao binafsi
Amesema kutokana na miradi mingi ya maendeleo ambayo imetekelezwa na serikali ya CCM wapinzani wao wanatumia mkataba wa bandari kama ajenda ya kisiasa kwakuwa nchi inaeleeka kwenye uchaguzi.
Amesema kuwa uwekezaji huo ukianza kufanya kazi serikali itaweza kuongeza makusanyo kutoka trioni 7 hadi trioni 26 fedha itakayochochoea ukuaji wa uchumi wa watanzania.
Amewataka watanzania kuendelea kumuamini Rais Dkt. Samia kwa namna anavyoiendesha nchi na maendeleo ambayo yanapatikana huku akifafanua kuwa hakuna Bandari iliyouzwa hata moja.
Post A Comment: