Tumaini Mafie,ARUSHA
Maendeleo ya Teknolojia hususani ya akili bandia yasiwe Chanzo Cha kuharibu maadili ya Kitanzania Vijana kwa wazee wametakiwa kujiepusha na uvunjifu wa maadili.
Hayo yameelezwa na mdau wa ASASI za Kiraia na mshiriki katika Mkutano wa Asasi za Kiraia AZAKI unaoendelea katika mkoa wa Arusha ambapo umewakutanisha mashirika yasiyoyakoserikali pamojaa na ASASI za Kiraia kutoka nje na ndani ya Tanzania.
Akizungumza katika Mkutano huo mmoja wa washiriki wa Mkutano huo Amani Golugwa ambaye pia ni katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini amesema Kila mtu anapaswa kulinda maadili ya Kitanzania.
"Teknolojia zipo na zinaendelea kukua Kwa kasi ,lakini siyo Kila unachokiona unatakiwa kujifunza au kukichukua katika mitandao ya kikamii.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Mwamvuli wa mashirika yasiyo ya kiserikali Jumuiya ya Afrika Mashariki Daniel Lema amesema wajumbe wa Asasi za Kiraia wameenda kujifunza jumuiya hiyo inafanya kazi gani lakini namna gani wanaweza kushirikiana katika kutatua changamoto za jamii.
Amesema teknolojia ya akili bandia inamchango mkubwa katika Jumuiya ambapo amesema vitu vingi katika Jumuiya hiyo hufanyika Kwa njia ya mitandao au kidijitali.
Naye mshiriki Mwingine kutoka Zanzibar Hija Shamte amesema hiyo ni fursa Kwao kujifunza in ni. katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hususani Katika Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Asasi za Kiraia nchini Dk. Liliani Badi amepongeza Jumuiya ya Afrika Mashariki Kwa kuendelea kushirikiana na Asasi za Kiraia hasa katika Kuruhusu utoaji wa maoni kutoka Kwa Asasi hizo.
Post A Comment: