Na Mary Margwe, Ruangwa


Katika suala la kukabiliana na ajira, Kampuni ya Elianje Genesis Kampani Limited imefanikiwa kuajiri zaidi ya wafanyakazi wapatao 200 wengi wao wakiwa ni Vijana kutoka Mtwara na Lindi.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Meneja wa Kampuni ya Elianje Genesis Kampani Limited Philbert Simon Massawe inayojishughulisha na Uchimbaji wa madini mbalimbali katika eneo la Namungo, pamoja na Namkonjera Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi

Massawe amesema katika jitihada za kukabiliana na suala la ajira kwa Vijana hususani katika maeneo yanayozunguka Mgodi wa Elianje Genesis Kampuni hiyo imefanikiwa kuajiri zaidi ya wafanyakazi wapatao 200 wameajiriwa na Kampuni hiyo.

" Kupitia jitihada zetu, tumeajiri zaidi ya wafanyakazi wapatao 200 ambao wanapata huduma zote za msingi Kwa maana ya Bima ya afya kutoka NHIF na pia wanachangia mfuko wa hifadhi za jamii ( NSSF) hii ni Kwa waliokidhi vigezo, hawa  wote wamechangia Kwa kiasi kikubwa katika kuleta Maendeleo kwa eneo hili na hatimaye kuinua uchumi wa watu katika kata wanazotokea" amesema Meneja Massawe.

" Tunaelewa umuhimu wa kuwekeza katika jamii yaani rasilimali watu,nanndio maana tumewajengea uwezo wafanyakazi wetu ili waweze kufanya kwa ufanisi na katika Mazingira ya usalama mkubwa" ameongeza Massawe.

Amesema kampumi ya Elianje Genesis inayostawi kwa kasi  imedhihirisha dhamira yake thabiti katika uchimbaji  wa Madini mbalimbali hapa nchini ikiwemo Madini ya Graphite, Nikei, Chuma, Green Garnet, Dhahabu, na Copper.

Kufuatia hilo ameishukuru Serikali kwa kuwajengea Mazingira mzuri ya kuwawezesha kufanya Biashara kikamilifu bila matatizo, ambapo hadi Kampuni hiyo imeweza kufika hatua ya kuajiri wafanyakazi 200 hadi sasa, ukilinganisha Kampuni hiyo ilipoanza kazi 2016 ilikua na Wafanyakazi 10.

" Kampuni yetu ya Elianje Genesis Kampani Limited ilianza Mwaka 2016 na kusajiriwa 2020 hukunikiwa na Wafanyakazi 10, ambapo kwa sasa Kampuni imefikia kuajiri wafanyakazi zaidi ya 200 hili ni jambo kubwa sana katika jamii, maana bila uwepo wa Kampuni hii maeneo haya Vijana na Wafanyakazi wengine wangekuaniatika Mazingira gani, lakini hapa  wanafanya kazi na kuleta Maendeleo nmajumbani kwao" amesema Massawe.

Akielezea baadhi ya mafanikio yaliyofanywa na Kampuni hiyo Kwa jamii Massawa amesema kampumi ya Elianje Genesis imeweza kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuunganisha miundombinu nya barabarani za Vijiji na Vijiji, kujenga madarasa katika shule zinazozunguka Mgodi pamoja na  kuchimba kisima cha maji kwa jamii.

Kufuatia kuwepo kwa baadhi ya changamoto Massawe ameiomba Serikali kuweza kuongeza nguvu katika suala la kukatika katika Kwa umeme, ambapo anapokosa umeme wanalazimikakuingia gharama kubwa kupata nyenzo mbadala ya umeme kama nishati ya diseli na petroli wakati mwingine huwa hazipatikani kwenye vituo vinavyouza mafuta hayo.

Kufuatia hilo Massawe ameiomba Serikali kuendelea kuwashika mkono katika kukabiliana na changamoto hiyo ili waweze kukabiliana nanoda hizo mpya walizopata kwenye Maonyesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji yaliyofanyika katika Viwanja vya Soko Jipya Kilimahewa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi

" Licha ya kuwa Bado Kuna mapungufu machache  hatuwezi kuilaumu Serikali moja kwa Moja, bali tunashukuru kwani awali hatukua na nguvu kubwa ya umeme ambapo ulikua unakatika karibia siku 5-7 Kwa wiki, lakini kwa sasa Serikali imepigwa hatua kubwajapo Kuna mapungufu machache, niiombe Serikali yetu chini ya Rais wetu mchapakazi kwelikweli Dkt.Samia Suluhu Hassan kuongeza nguvu kwa upande wa nishati ambapo ndio zimeweza kutufikisha hapa tulipo" amesema Massawe

Hata hivyo Massawe ameongeza kuwa Kampuni hiyo imejikita zaidi katika kuboresha vitendea kazi ili kuweza kuirahisishia kazi Kampuni hiyo kwa kuwepo kwa Vifaa Kwa kisasa vinavyowawezesha kufanya  kazi Kwa ufanisi  ikiwa ni pamoja na Excavator za kutosha, gari kubwa ( Malori) ya kutosha ambayo tayari yako yanafanya kazi ya kukamilisha
 tenda ambazo wamezipata.

Share To:

Post A Comment: