DENIS CHAMBI, TANGA.

JESHİ La Polisi Mkoa wa Tanga limewafikisha Mahakamani watu 5 wakazi wa Msomera wilaya ya Handeni mkoani hapa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa Mifugo huku likiwakamata wengine wawili raia wa Kenya waliokuwa wakijihusisha na wizi fedha kwenye magari.

Akitoa taatifa leo september 21,2023  kwa  waandishi wa habari kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga  ACP Almachius Mchunguzi alisema kuwa raia hao wa Kenya waliokuwa wakijihusiha na wizi wa fedha na mali mbalimbali za watu waliokuwa wakitoka benki  tayari wamefikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

"Katika oparesheni mbalimbali ambazo tumeendelea nazo tumekamata watu ambao wamekuwa wanajihusisha na wizi wa mifugo ambao ni Kaigwa Matapeli (26),  Mtemi Makulea (23),  Daniel Zakayo (24) ,  Adam Yusuph (23)  wote wakiwa ni Wamasai wakazi wa Msomera pamoja na  Halid Said mkazi wa kijiji cha Mbangu wote wamefikishwa mahakamani ili waweze kujibu tuhuma zinazo wakabili" alisema Kamanda Mchunguzi.

"Tulifanikiwa kuwakamata watu wawili raia wa Kenya ambao wamekuwa wakifanya uhalifu wa pesa na mali za watu katika  magali yao wamekuwa wakivizia watu wakitoka  benki wanafungua na wanachukua fedha watuhumiwa hawa wamekuwa wakitumia gari aina ya İST kutekeleza wizi wao walihojiwa na kukiri kufanya makosa hayo na tayari wamefikishwa Mahakamani ili waweze kujibu tuhuma ambayo wanakabikiana nayo" aliongeza

Aidha kamanda huyo alisema kuwa  katika kipindi cha mwezi mmoja september 2023 jumla ya watuhumiwa 6 wamehukumiwa kutumikia vifungo vyao hii ni mara baada jeshi hilo kukamilisha upelelezi wa makosa yaliyokuwa yanawakabili.

"Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga limefanikisha kesi 6 ambazo mahakama imeweza kuwatia hatiani watuhumiwa 9 ambao ni  Ally Sabala amefungwa jela mwaka mmoja kwa kosa la kuaminiwa , Joshua Madenge  amefungwa mwaka mmoja ,  Christopher Mazengo amefungwa jela miezi 6, Muya Chambo amefungwa jela miezi 6 wote wakipatikana na pombe aina ya Moshi,    Daniel Simon amefungwa jela miaka 12 kwa kosa la kupatikana Bangi Rashid Faki wote wakifungwa miaka 12. 

"Wengine ni  Selemani Ally ambaye amefungwa miaka mitatu kwa kosa la kupayikana na bangi , Ramadhani Salimu amefungwa miaka 30 kwa kosa la kuvunja nyumba usiku na kuiba na watuhumiwa wote wamepata kile ambacho wamestahili kwa mujibu wa sheria"

Pamoja na hayo Kamanda Mchunguzi amebainisha kuwa jeshi hilo linaendesha msako maalum wa kuwatafuta wale wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria ambapo amewataka kuzisalimisha kabla ya kufika october 31, 2023.

"Tumekuwa tukiendesha zoezi la kuwataka wananchi wasalimishe silaha  haramu au wanazomiliki kinyume cha sheria  zoezi hili lilianza tarehe 1 september ambalo litaisha  30 October  2023 niwatake wananchi ambao wanamiliki silaha visivyo halali sasa hivi wanaruhusiwa kuzisalimisha  lakini baada ya hapo kuna oparesheni kali kuwakamata wale wote  wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na isivyo halali" alisema.

Share To:

Post A Comment: