Hifadhi ya Ziwa Mnayara ni hifadhi ya Taifa ya Tanzania iliyo maarufu sana nchini kwa simba wanaopanda juu ya miti. Aina hii ya simba hupatikana ndani ya hifadhi hii pekee barani Afrika.

Hifadhi hii iko umbali wa kilomita 126 kutoka Arusha Mjini ikiwa na ukubwa wa Kilomita za mraba 325, ukubwa unaokaribiana na Nchi ya Maldives. Jina la hifadhi hii limetokana na mmea wa mnyaa ambao katika lugha ya Kimasai hujulikana kama Elmanyarai na sehemu kubwa ya hifadhi hii ni Ziwa Manyara.

Hifadhi hiyo iko katika Mkoa wa Arusha na Mkoa wa Manyara. Hata hivyo, mikoa hii miwili ya utawala haina mamlaka juu ya hifadhi bali hifadhi hii inasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Tanzania.

Licha ya umaarufu wa Ziwa Manyara lakini baadhi ya dosari zimeingia baada ya kutokea vurugu unyanyasaji katika ziwa hilo baada ya wavuvi saba kujeruhiwa na wawili kudaiwa kufariki kuzamishwa kwenye maji na Askari wa hifadhi ya Ziwa Manyara.

Baraka Samweli ni mvuvi katika Ziwa Manyara ambaye Mkazi wa Mto wa Mbu Wilayani Monduli amekiri kutokea vurugu na unyanyasaji katika eneo lao la kujitafutia ridhiki ambapo anaeleza vurugu hizo zimetokana na uzembe wa uwajibikaji kati ya Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu ambaye alikaidi kuitisha kikao kati wa wavuvi hao na watendaji wa Hifadhi ya Ziwa Manyara kwaaajili ya kutatua mgogoro wa mpaka kati yao na Ziwa Manyara.

“Kabla ya kutokea vurugu hizi tuliomba kuonana na watu wa Tanapa ili tueleze changamoto zetu lakini Mtendaji alitukwepa kila tukimweleza anakaidi na ndio haya yaliyotokea na hatujui wenzetu wanaodhaniwa kuzamishwa majini wapo wapi hadi sasa tunavyoongea’’ Alisema Samwel

Naye Jenipha Godfrey ambaye ni mfanyabiashara wanaoununua Samaki hao katika eneo la feri amesema aliona wavuvi wawili wakikimbia na kudai wenzao wamezamishwa majini ndipo mayowe yalipoanza na kuepelekea vurugu hizo zilizosababisha vifo na majeruhi kadhaa waliopigwa risasi katika maeneo mbalimbali ya miili yao.

“Hata kama wavuvi wamefanya makosa kwanini Askari wa Tanapa waliokuwa zamu wamewazamisha na hadi sasa miili yao haijapatikana ,hili suala linatakiwa kulaaniwa kwa undani kwani kuna biashara wanazofanya hawa askari dhidi ya wavuvi na sasa polisi waseme waliozamishwa wamepatikana au la” Aliongezea

Kutokana na ghasia hizo watu wawili walifariki na saba kujeruhiwa ambapo walilazwa katika hospitali wakati wakiendelea kupatiwa matibabu na upelelezi wa shauri hilo unaendelea,  ili kubaini walioanzisha vurugu hizo, pamoja na kuchunguza madai ya kuzamishwa kwa wavuvi wenzao katika maji na endapo wakibaini ukweli kulingana na ushahidi watu hao  watafikishwa mahakamani.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo alisema tukio hilo lilitokea katika kitongoji cha Magomeni Kijiji cha Jangwani eneo la Mto wa Mbu wilayani Monduli  wakati askari wa Hifadhi  ya Manyara wakiwa  katika doria ya kawaida katika eneo la Ziwa Manyara, ambapo walikamata wavuvi watatu waliokuwa wakivua samaki katika  maeneo  yaliyozuiliwa kwa ajili ya uhifadhi.

“Wakati askari hawa wakiwa doria ghafla walijitokeza wavuvi wengine na kuzusha vurugu iliyosababisha askari hao wa uhifadhi,  kushindwa kuwachukua watuhumiwa hao na kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi, ambapo umati wa watu hao walikwenda Ofisi ya Kijiji cha  Jangwani na kufanya uharibifu mkubwa, katika ofisi hiyo ya serikali kwa kuvunja madirisha pamoja na kuchana bendera ya Taifa na kuondoka nayo, kwa madai  kuwa wavuvi wenzao wamezamishwa  maji ziwani wakati wanakamatwa na askari wa uhifadhi”

“Kundi kubwa la wananchi wa eneo hilo, liliandamana na kufanya uharibifu wa ofisi za serikali uharibifu huo ulipelekea  kuchanwa kwa  bendera ya Taifa kwa madai ya kuzamishwa wavuvi wawili kwenye ziwa  Manyara na askari wa Hifadhi ya Manyara. Kutokana na vurugu hizo watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.Baada ya uharibifu huo kundi hilo, lilielekea ofisi na makazi ya askari wa TANAPA yaliyopo Mto wa Mbu na kuharibu magari kwa kutumia marungu na mawe pamoja na kupanga mawe barabarani, kuzuia watumiaji wengine wa barabara wasiendelee na shughuli zao” Alisema


Baada ya vurugu hizo Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, lilitoa onyo kali kwa  baadhi ya watu wenye tabia  ya kupambana na vyombo vya dola, ambao kimsingi  wamepewa dhamana ya kulinda maisha ya watu na mali zao pamoja  na usalama wa nchi, kwani inaweza  kusababisha madhara makubwa.

 

Alishauri endapo kuna changamoto yoyote zipo taratibu  nzuri za kufuata, kuliko kufanya vurugu na kujichukulia sheria  mikononi, kwa  kupambana na vyombo  vilivyopewa mamlaka kisheria ya kulinda maisha ya watu, mali zao na rasilimali za Taifa.


Kwa upande wao Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema kuwa uchunguzi wa tukio wa matukio yanayojitokeza katika Ziwa Manyara unaendelea na ukikamilika watu wanajihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua zinazostahiki.

 

Aidha wamewasihi wananchi wnaofanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo kuheshimu sheria za uhifadhi na rasimali zilizopo nchini kwani wananchi wanavyong’oa alama za mipaka iliyowekwa na kuingia hifadhini ni hatari na kinyume cha taratibu za Nchi.

 

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika hilo TANAPA William Mwakilema amesema vitu vingine vinakuzwa na kuongeza kuwa suala la wananchi kuzamishwa kwenye maji ni suala la kusadikika lakini vyombo vya ulinzi bado vinaendelea na uchunguzi wa suala hilo.


Kamishna Mwakilema ameeleza kuwa katika vurugu zilizotokea hapo awali mtu mmoja alipoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa vibaya, katika vurugu zilizotokea kwenye Kitongoji cha Magomeni, Kijiji cha Jangwani eneo la Mto wa Mbu Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha, baada ya kundi kubwa la wananchi wa eneo hilo, kuandamana na kufanya uharibifu wa ofisi za serikali .


Ameendelea kueleza kuwa uharibifu huo ulipelekea kuchanwa kwa bendera ya Taifa kwa madai ya kuzamishwa wavuvi wawili kwenye Ziwa Manyara na askari wa Hifadhi ya Manyara ambapo  kutokana na vurugu hizo watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.


Alisisitiza sheria za uhifadhi lazima zilindwe hivyo wananchi waheshimu sheria zilizopo kwani upelelezi unaendelea kwa jeshi la polisi ikiwemo kuchunguzamadai ya wavuvi kuzamishwa ndani ya maji na ukweli ukibainika waliohusika watachukuliwa hatua.






Share To:

Post A Comment: