Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi
wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imekemea tabia za baadhi ya wazazi
na walezi kufanya ukatili kwa kuwanyanyasa watoto.
Wameyasema hayo baada ya kupokea taarifa
na kuwatembelea watoto wanne aliotoroka nyumbani kwao Ushirombo Mkoani Geita na
kukimbiania kwa babu yao kata ya Ibadakuli Mkoani Shinyanga, kwa kile kinachoelezwa kutezwa na
mama yao wa kambo.
Babu wa watoto hao, mzee Mwandu Nangi
Malaba mkazi wa kitongoji cha Wiligwamabu kijiji na kata ya Ibadakuli Manispaa
ya Shinyanga amesema watoto hao wanne walitoroka nyumbani kwao toka mwezi Julai
Mwaka huu 2023 ambapo mpaka sasa takribani miezi mitano hawajahudhuria shuleni.
Mzee Mwandu Malaba pamoja na mambo mengine
ameiomba serikali kuingilia kati changamoto hiyo ili watoto waweze kupata haki
yao ya elimu kwa kuhakikisha wanaendelea na masomo kwani mpaka sasa hakuna
juhudi zozote zinazofanyika kwa wazazi.
“Naiomba
serikali iingilie kati changamoto hii iweze kunisaidia wajukuu zangu waendelee
na shule maana mimi sina mawasiliano na mama yao mzazi ila baba yao ambaye
alishaoa mwanamke mwingine alipiga simu siku moja tu akiwaulizia kama watoto
wamefika salama toka siku hiyo tukipiga namba yake haipatikani”.
“Mtoto
wa kwanza anayekadiriwa kuwa na umri wa Miaka 15 alikuwa akisoma kidato cha
kwanza shule ya Sekondari Businda Mkoani Geita, mtoto wa pili mwenye umri wa
miaka 12 alikuwa akisoma darasa la sita (6) shule ya msingi Businda, mtoto wa
tatu mwenye umri wa miaka 8 alikuwa akisoma darasa la kwanza shule ya msingi
Businda pamoja na mtoto wa nne mwenye umri wa miaka 4 yeye alikuwa bado
hajaanza kusoma”.amesema Mzee Mwandu
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa
SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, ambaye ni Mwenyekiti idara ya maadili Bwana
Solomon Najulwa pamoja na katibu wa
SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya wamelaani tabia zinazofanywa na
baadhi ya wazazi na walezi katika jamii kuwafanyia ukatili watoto kwa kuwanyima
haki zao za msingi ikiwemo haki ya elimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha
Wiligwamabu amekili kupokea taarifa za watoto hao toka Mwezi Julai Mwaka huu
2023.
Post A Comment: