..............................................
Na Said Hamdani, LINDI.
MKAZI wa
Kijiji cha Makangaga, Kata ya Kiranjeranje,Wilaya ya Kilwa,Mkoa wa Lindi,Salehe
Lihanzi (47) amelazwa Hosptalini akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya kukatwa
mapanga maeneo mbalimbali ya mwili wake na watoto wa kufukia wa mke wake.
Tukio hilo linaelezwa kutekelezwa na vijana hao
August 31 mwaka huu saa 7;00 mchana,alipokuwa shambani akilinda mazao yake
yasishambuliwe na wanyama waharibifu.
Lihanzi amelazwa wodi namba sita katika Hosptali
ya Sokoine,nl mkoani Lindi na amewataja watoto hao kuwa ni Ally Halfani na
Hassani Mbulula.
Amesema siku hiyo akiwa shambani akilinda mazao
yasiliwe na wanyama waharibifu alifuatwa na vijana hao wakiwa na mapanga na
fimbo mikononi mwao.
Lihanzi amesema baada ya kufika mahali
aliposimama alikatwa panga mguu na mkono
wa kulia na mtoto mkubwa Ally Halfani huku mdogo wake Hasani akimpiga na fimbo
kichwani.
Ametaja sababu ya yote hayo ni kuwataka watoto
wale kurejesha vitu walivyochukuwa kikiwemo kitanda cha mbao chenye ukubwa wa
futi 5 kwa 6.
Amesema licha ya kuwaeleza kurejesha vitu hiyo,
suala hilo alilifikisha kwa mama wa
watoto hao Ashura Mbunda ambae ni mke wake na kwa bibi yao Zaria Omari ambapo
walikubali kuvirudisha.
Amesema ndipo August 30, 2023 saa 7;00 mchana akiwa shambani
vijana hao walimfuata na kuanza kumshambuli na kumsababishia maumivu makali.
Mkulima huyo amesema baada ya watoto hao
kumfanyia ukatili huo waliondoka kuelekea Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji na kueleza kule walicho mfanyia.
"Nilipowaona wanakuja sikuwa na hofu nao
wala kudhani wanakuja kundhuru,"alisema Lihanzi.
Lihanzi amesema mtu wa kwanza kufika eneo la
tukio ni mama mkwe wake Zaria Omari na kumuomba aende kijijini kuwapa taarifa
ndugu zake kwa kile kilichomkuta.
Mkulima huyo amesema baada ya ndugu kufika eneo
hilo walimchukua na kumpeleka Zahanati ya Kiranjeranje,lakini kutokana na uzito
wa tatizo wakalazimika kumpeleka Hosptali ya Mkoa Sokoine,iliyopo mjini Lindi.
Amesema tayari askari polisi wamefika Hosptali
kuchukuwa maelezo yake kwa ajili ya ya kuyafanyia kazi.
Mganga Mfawidhi Hosptali ya Sokoine,mkoani Lindi,
Alexander Makalla amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo August 30, 2023 saa 2;00
usiku.
Makalla amesema mgonjwa huyo ameshambuliwa na
kitu chenye ncha kali mguuni na mkono wa kulia na kichwani na hali yake
inaendelea vizuri kutokana na huduma za matibabu anayoyapata
"Mteja wetu amejeruhiwa mguu na mkono wa
kulia na kichwsni" alisema Makalla.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi,Pili Mande
amekiri kuwa na taàrifa hiyo na kueleza wanaendelea kuifanyia kazi.
Post A Comment: