Waziri wa Madini Anthony Mavunde amewahikishia watanzania wengi zaidi kushiriki katika kutoa huduma na kuzalisha bidhaa ambazo zitatumika kwenye sekta ya madini kupitia mpango wa ushirikishwaji wananchi kwenye sekta ya madini(_Local content_).
Waziri Mavunde kayasema hayo leo eneo la Bombambili,Mkoani Geita wakati akifungua mdahalo wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini (Local Content) ambao umeshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo watanzania watoa huduma kwenye migodi mikubwa nchini.
“Tunamshukuru sana Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kupitia sera na sheria mbalimbali ambazo zimeendelea kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya madini.
Tutaendelea kusimamia sheria na kanuni ipasavyo ili kuongeza wigo wa ushiriki wa watanzania wengi kwenye kutoa huduma na kuzalisha bidhaa zitakazotumika kwenye sekta ya madini.
Tunahitaji kuona watanzania wengi zaidi wanashiriki katika sekta ya madini,na serikali itasimamia kuhakikisha ushiriki wa watanzania kikamilifu kwa kuwajengea uwezo na kuwaunganisha na taasisi za fedha kwa ajili ya mitaji, hivyo nachukua fursa hii kutoa rai kwa Watanzania kuchangamkia fursa hii.
Sheria ya madini Sura ya 123, kifungu cha 102 kinataka makampuni ya madini kutoa kipaumbele kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa na watanzania au kampuni za kitanzania.
Kifungu hiki pia kina kinaendana na matakwa ya Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania (Local Content Regulations) ambazo zilitungwa mwaka 2018 na kufanyiwa marekebisho 2019 na 2022.
Kanuni hizo pia zinataka makambpuni hayo kutoa kipaumbale kwa watanzania na Kampuni za kitanzania. Lengo ni kuongeza ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya madini”Alisema Mavunde
Mdahalo huu ni muendelezo wa maonesho ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 30.09.2023.
Post A Comment: