Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini.Joseph Musukuma akizungumza na Wananchi wa Kata za Nzera na Rwezera wilayani Geita katika mkutano wa hadhara alioufanya jana mkoani humo.
......................................
Na Victor Bariety, Geita
BAADHI ya Wananchi wa Kata za Nzera na Rwezera
wilayani Geita wamesema wanalazimika kusajili line kwa kutumia vitambulisho vya
Taifa vya watu wengine kwa kuwa zoezi la
uandikishaji liliwapita kushoto na kuiomba serikali iangalie uwezekano wa
kurudia zoezi hilo ila wasije wakakumbana na mkono wa sheria.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, kwenye mikutano ya hadhara ya Mbunge wa jimbo la
Geita Vijijini.Joseph Musukuma,iliyofanyika kwenye kata hizo wananchi hao
wamesema wakati wa zoezi hilo maeneo mengi ya jimbo lao hayakufikiwa jambo
ambalo limewasababishia usumbufu mkubwa hasa wanapohitaji huduma inayohusiana
na kitambulisho cha NIDA.
Akijibu kero hiyo,mbunge musukuma amemuomba
GHULAM kufikisha kero hiyo kwa Rais wa Tanzania Samoa Suluhu Hassan na
ikimpendeza zoezi hilo lirudiwe.
"Mheshimiwa mbunge,suala la NIDA linatutesa
sana wananchi,tunalazimika kusajili line kwa kutumia NIDA za watu,tunajua ni
kosa lakini tutafanyaje,serikali itusaidie zoezi hili litufikie wananchi wa
vijijini," alisema Mashaka Masele huku akishangiliwa.
Mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya soko
kuu la Nzera, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali, akiwepo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) Mkoa wa Geita , Nadra Ghulam kwa niaba
ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda.
Kwa upande wake mjumbe huyo wa NEC mbali na
kuahidi kufikisha kilio hicho panapohusika,aliwataka wananchi kuwa na imani na
serikali yao.
"Mheshimiwa mgeni rasmi,umewasikia
wananchi,hili zoezi la NIDA ni kero kubwa,wakati wa uandikishaji,wananchi hawakujua
umuhimu wake lakini kwa sasa kila wanakoenda wanatakiwa wawe na NIDA ndio maana
wameanza kuona umuhimu wake nikuombe kamwambie mama yetu Rais Samia ikimpendeza
hili zoezi lirudiwe upya,wananchi wanapata usumbufu mkubwa kwa kukosa
NIDA"alisema Musukuma huku akishangiliwa na wapiga kura wake.
"Ndugu wananchi niwaombe tu,tuwe na imani na viongozi wetu na tuwasifie pale wanapofanya vizuri,sio tusubiri mpaka waondoke ndio tuwasifie, "alisema Ghulam.
Post A Comment: