Mwishoni mwa mwaka 2022, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliridhia kutoa kiasi cha Shilingi Bilioni 160 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 8,000 vilivyoweza kupokea wanafunzi 400,000 wa Kidato cha Kwanza walioanza masomo mwezi Januari, 2023 ambao ni zao la Elimu msingi bila ada.
Serikali ya awamu ya sita wakati ikiendelea kujivunia mafanikio ya kujenga shule za Kata nchi nzima, Hali ipo tofauti katika Kata ya Mswakini ambako ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika kata hii umekamilika na majengo ya shule yameaanza kuchakaa na kuwa magofu. Hii ni baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kushindwa kuanza kutumia shule hiyo kwa kupeleka wanafunzi kwa ajili ya kuanza rasmi shule hiyo ambayo majengo yote ya muhimu yakiwa yamekamilika.
Mswakini ni Kata iliyopo Katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha yenye Vijiji Vitatu (3) na Vitongoji kumi na mbili (12). Kata hii ipo mpakani mwa Mkoa wa Arusha na Manyara, na katika mapitio ya Wanyama pori wa Hifadhi ya Tarangire na Hifadhi ya Ziwa Manyara.
Naituuy Mollel ni mama wa watoto watatu anasema kuwa kuanza kutumika kwa shule hiyo itakuwa jambo jema ili Watoto wao waweze kusoma shule ya kutwa na kuweza kurudi majumbani. Kwa sasa wanasoma mbali na makazi yao jambo ambalo linawawia gharama kutokana na hali yao ya kifugaji iliaridhiwa na mabadiliko ya tabia nchi.
“Sisi kama wananchi wa Kijiji hiki ambacho shule hii imejengwa tunashangaa kabisa kwanini shule imekamilika na pia tuliona Mwenge wa Uhuru ulikuja kuweka jiwe la msingi lakini cha kushangaza mpaka saasa majengo yamekamiliska shule haijaanza kutumika imekuwa kama kichaka sasa” Alisema Naituuy
Mosses Ngaitulo ni dereva wa usafirishaji wa pikipiki (Bodaboda) anaeeleza namna ambavyo walianza kujenga shule hiyo kwa kutumia nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha Watoto wao wanapata elimu ya sekondari kutokana na umbali wa Vijiji vyao kuwa mbalimbali.
Hata hivyo Mosses ameiomba serikali kufanya jitihada za makusudi kuifungua shule hiyo ifikapo Januari 2024 mwakani, ili kuepusha adha waipatayo wanafunzi wanaotoka katika kata hiyo, ambao alisema mbali na kutembea umbali mrefu, ndiyo wanafunzi kutafuta elimu ya msibngi kwani kuunguliwa kwa shule hiyo itakuwa chachu ya wanafunzi hao kupata elimu karibu.
Nanga Mollel ni Diwani wa Kata ya Mswakini ambapo anatueleza kuwa changamoto kubwa mpaka kutokuanza rasmi kwa shule ya mswakini ni kutokuwepo kwa maji na umeme sambamba na nyumba za watumishi katika shule hiyo.
Diwani anatueleza kuwa hali ya wanafunzi kwenda umbali mrefu kusaka elimu ya sekodari ni la muda mrefu kwani Halmahauri huwa inawapanga Watoto shule za mbali na makazi yao.
“Majengo yote yamekamilika na wakaguzi walishakuja kukagua, lakini kikwazo kikubwa mpaka ni nyumba ya Walimu na swala la maji na umeme ndio ambavyo vinachangia mpaka sasa shule hii kutokuanza kupokea wanafunzi lakini madarasa yote nane yamekamilika na maabara zimekamilika vyoo sambamba na jengo la utawala” Alisema Mollel
"Niombe serikali kuangalia na kufikisha maji kwa wakati pale shuleni ili ianze kutumika maana pale changamoto kubwa ni maji na sio kitu kingine" Aliongezea
Ikumbukwe Serikali katika mwaka wa fedha 2021/22, ilitoa jumla ya Shilingi Bilioni 108 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya za Kata 231 ambazo zilitarajiwa kupokea wanafunzi mwezi Januari, 2023.
Post A Comment: