Wachimbaji nchini Tanzania kuwezeshwa mtaji na Benki Kuu ya Tanzania kwa madhumuni ya kuongeza uzalishaji wa dhahabu nchini ambayo itanunuliwa na Benki kuu ya Tanzania(BOT).

Hayo yamesemwa leo Wilayani Bukombe,Mkoani Geita na Waziri wa Madini Anthony Mavunde wakati akihutubia mkutano wa wananchi wa Bukombe waliojitokeza kwa wingi kumpokea Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Dotto Mashaka Biteko.

Waziri Mavunde amesema kwamba serikali inaandaa mpango kupitia mfuko wa dhamana (_Export Credit Guarantee Scheme_)ili kuangalia namna ambavyo itawasaidia  wachimbaji wadogo ili wapate fedha, wachimbe na kuuza kwenye viwanda vya kusafisha dhahabu ili itakapo chujwa iweze kuuzwa kwa Benki Kuu,ambapo amewapa wataalamu wa Serikali siku 5 kuhakikisha wanakamilisha mpango huo ili kutekeleza maagizo ya Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Benki kuu Tanzania (BOT)kununua dhahabu kwa wachimbaji wa Tanzania kwa utaratibu mzuri.

Maelekezo hayo yaliwekwa msisitizo zaidi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Dotto Mashaka Biteko jana wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini katika eneo la Bombambili Geita na kuwataka Wizara ya Madini na Benki Kuu Tanzania(BOT) kuharakisha zoezi la ununuzi wa dhahabu wa kilo 6000

Share To:

Post A Comment: