Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed O. Mchengerwa amesema katika maombi maalum ya fedha za uimairshaji wa huduma za Afya jumla ya Vituo vya Afya 214 vitajengwa nchi nzima.

Kati ya Vituo hivyo Halmashauri ya Wilaya na Nanyamba watapata kituo cha Afya kimoja ambapo watakua na jumla ya vituo vya Afya 6 na Hospitali ya Wilaya 1 itakayosaidiana na zahanati ambazo kwa pamoja zitatoa huduma ya Afya katika Halmashauri hiyo.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati akijibu hoja za Wananchi wa Halmashauri hiyo wakati Mhe. Rais aliposimama kusalimia wananchi wa Nanyamba katika eneo la Mahakama leo tarehe 16.09.2023.

Amesema “Mhe Rais tulileta kwako maombi maalum ya  fedha za nyongeza kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya na ufedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Agfya 214 na kimoja kati ya hivyo kitajengwa hapa ili kuendelea kuimarisha huduma za Afya’

Nikijibu hoja ya Wananchi wa Nanyamba ambao wamehoji kuhusu uhaba wa Wawatumishi wa Elimu na Afya ni kuwa kupitia Ajira Mpya ulizotupatia Nanyamba watapa Jumla ya Watumishi 76 ambao watasaidia kupunguza changamoto hiyo.

Tatizo hilo la upungufu wa Watumishi tunalitambua na kwa Kibali cha Ajira ulichotupa hapa Nanyamba wataletwa watumishi 76 wa kada zilizombwa ili kusaidia katika maeneo hayo ya Elimu na Afya.

Halkadhalika kupitia TARURA tutaendelea kuboresha miundombinu ya barabara za Nanyamba.

Share To:

Post A Comment: