Na Mwandishi Wetu - Zanzibar 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdulla amewapongeza watumishi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),kwa kufanya kazi ya kuleta mageuzi kwenye Sekta hiyo ikiwemo kusimamia miundombinu ya Mawasiliano ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo cha Taifa -cha kuhifadhi data kimtandao NIDC.


Ameyasema hayo leo Septemba 23,2023 Visiwani Zanzibar wakati wa kikao kazi Cha Bodi ya wakurugenzi na Menejimenti ya TTCL chenye lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa kuzingatia maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla.



Abdulla amesema Shirika hilo limepewa dhamana kubwa ya kusimamia miundombinu ya kimkakati ya Mawasiliano ambayo ni Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo Mahiri Cha kuhifadhi data kimtandao hivyo inapaswa kuwajibika kupanga namna bora ya kuhakikisha miundombinu hiyo inatunzwa kwa malengo na tija iliyokusudiwa.


"Tumieni kikao hiki kujadili changamoto zinazolikabili Shirika katika utekelezaji wa majukumu yenu na mpate suluhusho kwa changamoto zote zilizopo,"amesema Abdulla



Pamoja na hayo ameielekeza Bodi hiyo kuhakikisha ujenzi wa kilometers 1600 za mkongo wa Taifa zinakamilika ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa vituo vipya 15 vya kutolea huduma za Mkongo kwa lengo la kuongeza wigo wa utoaji wa huduma wa Mkongo wa Taifa hadi ngazi za Wilaya.


Aidha, ametaka Bodi hiyo kutumia fursa za uwepo wa Mkongo wa Taifa kufungua biashara nchi za jirani ikiwa ni pamoja na kuwezesha maeneo 50 muhimu ya Umma katika miji mikuu kupata huduma ya Mtandao.


"Hakikisheni mnafanya tafiti na kuishauri Wizara namna bora ya kushusha gharama za huduma za Mkongo kwa tija Ili kuvutia wateja wengi zaidi,pia fanyeni tafiti za kuibua huduma zinazoambatana na matumizi ya faiba,"amesema Abdulla

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Bi.Zuhura Sinare Muro, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa kuendelea kuwekeza katika Miradi ya Mawasiliano na Ile ya miradi ya miundombinu ya Kimkakati ambapo katika Mwaka huu wa Fedha 2023/2024 imewekeza zaidi ya Trilioni 1 na kupitia uwekezaji huo Shirika litaongeza Kasi katika kukamilisha Ujenzi wa mkongo wa Taifa na kuwafikia watanzania wengi.


"Niwashukuru pia Bodi na Menejimenti ya Shirika letu Kwa kuendelea kutekeleza majukumu Kwa ushirikiano Mkubwa lengo likiwa ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya Mawasiliano iliyo Bora,"amesema Zuhura
Katibu Mkuu WHMTH Bw. Mohammed Abdullah akifafanua jinsi TTCL ilivyopiga hatua katika kuhakikisha inafungua milango kidigitali Tanzania alipofungua Kikao Kazi cha Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TTCL kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Septemba 23, 2023
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano,na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdulla akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL ( Wa pili kulia) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw. Cecil Fransis (wa pili kushoto) na wajumbe wa Kikao Kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Septemba 23, 2023
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Mohammed KhamisAbdullah akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa  Bodi  ya TTCL wakati wa Kikao Kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Septemba 23,2023
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed KhamisAbdullah akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TTCL wakati wa Kikao Kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Septemba 23,2023


Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: