Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Toto Afya Kadi haijafutwa ila kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili ambapo utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh. 50,400 ili waingie wengi, wasio Wagonjwa na hivyo kuweza kuchangiana wachache watakaogua.
Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akijibu maswali mengi kutoka kwa wadau mbalimbali kupitia mtandao wa X leo, waliokua wakiuliza kuhusu Toto Afya Kadi.
“Bima ni Sayansi, wakate wengi wachangiane wachache watakaougua, Toto Afya Kadi haijafutwa, kilichobadilika ni utaratibu wa kuwasajili, utaratibu wa sasa ni kuwa Watoto wasajiliwe Shuleni kwa gharama ileile ya Tsh. 50,400 ili waingie wengi, wachangiane na wasiokuwa wagonjwa”. Amesema Waziri Ummy
Aidha, Waziri Ummy amesema Kwa sasa Toto Afya Kadi wamesajiliwa Watoto laki 2 tu, hivyo amewataka wazazi na walezi kuwakatia Bima ya Afya Watoto ili waweze kupata matibabu kwa urahisi na haraka pindi wanapougua.
“Naamini wakisajiliwa watoto japo asilimia 10 tu (Milioni 3) kwa utaratibu huu basi tunaweza kuhakikisha ustahamilivu na uendelevu wa fao hili, Sera ya Watoto wa umri chini ya miaka mitano au Watu wasio na uwezo kupata msamaha bado haijafutwa, Hospitali zote za umma zinaendelea kuhudumia Watoto wa umri chini ya miaka mitano kupitia utaratibu wa misamaha”. Amesema Waziri Ummy
Post A Comment: