Na Kassim Nyaki, Handeni.

Timu ya Makatibu wakuu wa Wizara za Kisekta katika mradi wa ujenzi wa Nyumba 5,000 kwa ajili Wananchi wanaohama kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wametembelea eneo la Mradi kukagua maandalizi ya ujenzi huo. 

Kiongozi wa timu hiyo ambae ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas ameeleza kuwa; 

“Serikali ilishaahidi kutekeleza na kumaliza ahadi hii, tumemaliza awamu ya kwanza iliyojumuisha Nyumba zaidi ya 500 ambazo wananchi tayari walishahamia.

.....tumekuja kukagua na kushuhudia maandalizi ya ujenzi wa nyumba 5,000, kila kitu kipo tayari makatibu wakuu wa Kila Sekta wameangalia maeneo yanayohusu Wizara zao ili kukiwa na changamoto ziendelee kutatuliwa wakati kazi inaendelea ili ikifika mwishoni mwa mwezi Machi, 2024 tuwe tumekamilisha Nyumba zote eneo la Msomera, Kitwai na Saunyi.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando ameeleza kuwa ujio wa Makatibu Wakuu kutembelea eneo la mradi wa nyumba 5,000 na kutoa maelekezo ya ujenzi Unaoanza tarehe 1 oktoba, 2023 tayari uongozi wa wilaya umeshajipanga kutekeleza maelekezo yote ya Serikali.

Mkurugenzi mtendaji wa SUMA- JKT Kanali Petro Ngata ameeleza kuwa Vikosi vya Jeshi kwa ajili ya utekelezaji wa  operesheni ya ujenzi huo vimeshafika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza kazi na watahakikisha inakamilika ndani ya miezi sita kama ilivyopangwa.







Share To:

Post A Comment: