Na. Asila Twaha, Iringa
Timu ya wanawake kuvuta kamba TAMISEMI imeanza vizuri kwa kuikaba koo Ras Kagera kwa kuishinda kwa pointi 2- 0
katika Michezo ya Shirikisho ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yalioanza leo, Mkoani Iringa.
Ushindi huo umepatikana baada TAMISEMI kupangwa kucheza na RAS Kagera ambapo timu ya RAS Kagera haikuonekana uwanjani.
Kocha wa Timu ya Kuvuta Kamba TAMISEMI Chediel Masinga amesema ushindi wao hauna shaka sababu umezingatiwa taratibu zote kutoka kwa uongozi kwa wao kushinda pointi 2-0.
Ameeleza kuwa timu hiyo imeonyesha nidhamu, juhudi na ushirikiano wakati wote wa michezo na inaendelea kufanya mazoezi.
Michezo ya Shirikisho ya Wizara na Idara za Serikali yameanza rasmi leo yanatarajiwa kufunguliwa kesho katika viwanja vya Samora Mkoani Iringa.
Post A Comment: