Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Miongozo ya Elimu Maalumu na Jumuishi,Leo Septemba 12,2023 Jijini Dodoma. |
Prof.Mkenda ameyasema hayo Leo Septemba 12,2023 Jijini Dodoma wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Miongozo ya Elimu Maalumu na Jumuishi.
"Masomo ya Elimu Jumuishi na Lugha ya Alama yatakuwa ni lazima endepo Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 itapitishwa walimu wote wanaoandaliwa Kwa ajili ya kwenda kuwafundisha wanafunzi katika Shule zetu hapa Nchini ili waje kusaidia katika utoaji wa Elimu Kwa watoto wetu wote na Wenye mahitaji Maalumu,"
Na kuongeza "serikali inaendelea na jitihada za Kuimarisha mfumo wa utambuzi wa wanafunzi Wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata elimu kwani nao wana haki sawa ya kupata Elimu kama wanafunzi wengine,"amesema Prof.Mkenda
Prof.Mkenda amesema miongozo hiyo iliyozinduliwa inakwenda kuakisi juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Kila mwanafunzi anapata Elimu sawa bila kujali hali yake na ndio maana hata wale wanafunzi waliopata ujauzito wakiwa Shuleni wameruhusiwa kurejea shuleni na kuendelea na masomo yao.
Kwa upande wake Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema kuwa maendeleo kweli katika nchi yeyote Ile hutegemea uwepo wa elimu bora kwa wote.
"hakuna taifa lolote lile Dunia lililoendelea bila kuboresha Elimu yake kwa watu wa makundi yote na ndio maana Serikali kupitia Wizara ya Elimu inaendelea kuboresha na kuongeza Miongozo mbalimbali lengo likiwa ni kuboresha mfumo wa elimu,"amesema Dkt.Mtahabwa
Naye Mkurugenzi wa Elimu Kwa Wenye Uhitaji Maalum wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Magreth Matonya amesema ametaja miongozo minne ya Elimu Maalum na Jumuishi iliyozinduliwa kuwa ni Mwongozo wa kwanza ni Shule Nyumbani (home Schooling). Mwongozo wa pili ni ziara majumbani,Mwongozo wa tatu ni ule wa Ubainishi wanafunzi wenye Mahitaji maalumu na Mwongozo wa Uanzishwaji na uendeshaji Shule/Vyuo vya wanafunzi wenye mahitaji maalum na Jumuishi (standards)
"Hii ni hatua kubwa kwa taifa letu kwani ni kwa mara ya Kwanza tunakuwa na miongozo stahiki inayowezesha utoaji wa Elimu Kwa wanafunzi Wenye mahitaji maalumu na sasa wanakwenda kupata elimu Kwa usawa hata kama wapo majumbani.
Akizungumza Kwa niaba ya Wazazi wa Watoto Wenye Mahitaji Maalumu Bi.Sharifa Mbarak amesema miongozo hiyo imekuja kukata kitu na kuondoa kilio Kwa wazazi na watoto Wenye mahitaji maalumu kwani Kwa sasa wanapata haki ya kusoma hata wakiwa nyumbani.
"Watoto Wenye mahitaji Maalumu ni kama walisahaulika kidogo ila kupitia muongozo huu naamini inakwenda kuwa suluhisho kwa hawa watoto kupata elimu wakiwa nyumbani sawa na wale waliopo shuleni,"amesema Bi.Sharifa.
Post A Comment: