Na Okuly Julius-Dodoma
Ameyasema hayo Leo Septemba 16,2023 Jijini Dodoma,katika hafla ya kutangaza washindi wa Tuzo ya watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida yenye hadhi ya juu kimataifa.
"Ili uwe Mkubwa lazima upimwe ama ushindanishwe na Watu wa kubwa ndio maana tumewapima watafiti wetu Kwa kuangalia machapisho yao yaliyochapishwa katika majarida makubwa ulimwenguni,"amesema Mkenda
Prof. Mkenda amesema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 1 zilitengwa katika bajeti iliyopota ya Mwaka 2022/23 kwa ajili ya zoezi hilo lenue lengo la kutoa hamasa kwa watafiti wa sayansi na Teknolojia nchini.
Ambapo Jumla ya machapisho 82 yalipokelewa kutoka Tanzania bara na visiwani huku 71 kati ya hizo zilitoka katika vyuo vya elimu ya juu vya umma na 11 vyuo binafsi.Hatua hii ni kabla ya wizara kuandaa orodha Maalum iliyowasilishwa kwa kamati.
Sayansi ya Afya Shirikishi ,Sayansi Asilia pamoja na Hisabati ndio nyanja Maalum zilizokuwa zimependekezwa kushindaniwa katika awamu ya kwanza ya shindano hilo huku dirisha la nyongeza Kwa awamu ya pili kwa nyanja za uhandisi na TEHAMA sanjari na sayansi kilimo na wanyama ikifunguliwa Leo Septemba 16,2023 na inatarajiwa kufungwa Oktoba 31,2023.
Hata hivyo wakati wa uhakiki wa machapisho 82 katika hatua sita pendekezwa na kamati ilio chini ya wizara hiyo ya Elimu , machapisho 63 pekee ndio yalio kidhi vigezo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo Prof.Yunus Mgaya, amesema machapisho 82 yaliopokelewa na kamati hiyo kutoka kwa watafiti wa taasisi za elimu ya juu za umma na binafsi kwenye maeneo ya afya, sayansi shirikishi, sayansi asilia na hisabati.
“Baada ya mchakato kukamilika machapisho 20 ambayo kati yake 10 ni mkondo wa sayansi asilia na hisabati na 10 kutoka mkondo wa afya ya sayansi tiba yamekidhi vigezo vya kupata tuzo,”amesma Prof.Mgaya
Kukamilika kwa hatua hiyo ni kutoa fursa ya ufunguzi wa nyongeza wa dirisha jingine kwa nyanja za uhandisi na tehama sanjari na sayansi kilimo na wanyama ili kukamilisha kiasi cha bilioni moja zilizokuwa zimetengwa katika mwaka wa bajeti wa 2022/2023.
Post A Comment: