Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha imemfunga kifungo cha maisha Shedrack Saitoti baada kukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka saba .
Akisoma hukumu hiyo leo septemba 26 mwaka huu Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Ngorongoro,Kohawa Magreth Mboya amesema kuwa Saitoti amekutwa na hatia baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na mtumiwa kukutwa na hatia hivyo kupelekea kupata adhabu kali ya kifungo cha maisha.
Nae Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mimutie Women Organization Rose Njilo amesema kuwa wao kama taasisi ya kutetea haki za wanawake na watoto wameishukuru Mahakama hiyo kwa kutenda haki kwani adhabu hiyo itarudisha maadili kwa jamii na kuwa fundisho kwa wengine wenye tabi la za namna hiyo .
Aidha Rose Njilo ameishukuru Women Fund Tanzania kwa kuendelea kuwa wezeshaji wa shirika la Mimutie katika kuibua Changamoto za Ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.
Wadau mbalimbali na wanaharakati walifika katika mahakama hiyo kusikiliza hukumu hiyo na kusema kwamba Mahakama hiyo imetenda haki kutenda haki kwa mshtakiwa kwani akusumbua mahakama kwamba akufanya tendo hilo la ulawiti kwa mtoto huyo wa miaka 7
Post A Comment: