Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika jana mkoani hapa. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatma Mganga.
.............................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ameziagiza Halmashauri kuimarisha
ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha mashine za kukusanya fedha ] POSS}
zisitumike feki.
Serukamba alitoa maagizo hayo wakati akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa
wilaya, wenyeviti wa halmashauri na wataalam mbalimbali katika kikao kazi
kilichofanyika jana mjini hapa.
Alisema kumekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa mapato na matumizi ya POSS
feki hivyo kuukosesha mkoa kupata mapato stahiki ambapo aliviomba vyombo vya
dola ikiwamo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa} TAKUKURU } kusaidia
kufanya uchunguzi kwenye mageti ya ukaguzi wa mazao yanayosafirishwa.
Aidha, Serukamba alisema Mkoa wa Singida unaweza ukawa kinara wa ukusanyaji
wa mapato, uhifadhi wa mazingira na usimamizi wa miradi iwapo tu watendaji
watafanya kazi kwa kujituma na kushirikiana badala ya kuyaachia baadhi ya
makundi kufanya kazi hizo.
'' Tukifanya kazi vizuri katika uhifadhi wa mazingira, ukusanyaji mapato,
ukamilishaji wa miradi kwa wakati na kuwa timu moja, siku moja tutakuwa namba moja kitaifa,'' alisema
Serukamba.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatma Mganga akizungumza kwenye kikao
hicho aliwaomba wakurugenzi pindi wanapopokea fedha za miradi kabla ya kuanza
kutekelezwa watoke ofisini na kwenda kujua bei za vifaa badala ya kwaachia watu
wa manunuzi pekee ambao wamekuwa na changamoto ya kuweka bei ya juu.
'' Miradi mingi imekuwa haikamiliki kutokana na fedha zilizotolewa na
Serikali kumalizika kabla haijaisha na hiyo inasabishwa kununua vifaa kwa bei
kubwa lakini wakurugenzi wakitoka na timu yao watawakuta wauzaji wa vifaa hivyo
kwa bei ya chini.'' alisema Mganga.
Mganga akitolea mfano alisema alipokuwa mkurugenzi wa halmashauri wakati
wanataka kutegeneza milango waliwaomba watu wa manunuzi wawape bei yao ambapo
wasema ni Sh.Milioni 72 na walipotoka kutafuta bei kwa watu wengine alikuwepo
wa Sh.Milioni 50 na mwingine Sh.Milioni 48 na hivyo kumpa kazi hiyo aliyekuwa na
bei ya chini ambaye alifanya kazi hiyo kwa viwango vya hali ya juu.
Katika hatua nyingine Mganga aliwaomba wakurugenzi hao kujenga tabia ya
kwenda kujifunza kwa wenzao ambao wanafakiwa kukamilisha miradi ya maendeleo
kwa wakati na kwa fedha zilezile walizopokea kama wao.
Alisema utakuta Serikali imetoa fedha kiwango sawa lakini katika
ukamilishaji wa miradi kwa fedha hizo hizo halmashauri zingine zinakamilisha
miradi iwe ya ujenzi wa shule au vituo vya afya na halmashauri nyingine utakuta
ujenzi wake upo hatua ya msingi.
Aidha, Mganga aliwahimiza watendaji hao kuhakikisha miradi hiyo inakamilika
kabla ya Agosti 9, 2023 ambapo ndio itakuwa kikomo cha fedha za bakaa na baada
ya hapo zitarudi Serikalini.
Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine wakurugenzi na wakuu wa wilaya walitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato na miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye wilaya zao.
Post A Comment: