Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule akimkabidhi T-shirt mwanafunzi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania).

 MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule ameipongeza Taasisi ya Fountain Gate Academy kwa kuamua kuwezesha katika elimu na kukuza michezo kwa vijana kupitia academy ya Fountain Gate Dodoma.


Akizungumza leo na waandishi wa habari leo Septemba 1,2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kumuaga binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania), Mhe. Senyamule amesema kazi ambayo inafanywa na taasisi hiyo kutoa elimu na kukuza vipaji vya michezo inaunga mkono jitihada za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ameweka nguvu kubwa katika sekta ya michezo, burudani, sanaa na fani mbalimbali ambayo imeweza kuwapa ajira na kuwanufaisha wanamichezo na wasanii mbalimbali.

Amesema Kipaji na michezo ni fursa kiuchumi na kuingiza fedha nyingi " mfano hai tunaona namna wanamichezo wengi leo walivyo matajiri hapa kwetu na nchi mbalimbali".

Aidha Mhe.Senyamule amempongeza binti Marry kwa hatua ambayo ameifikia na juhudi ambazo amezionesha na kupata fursa ya kupelekwa nje ya nchi kwaajili ya kuendeleza kipaji chake.

"Nenda ukaongeze elimu ya michezo huko nchini Hispania ili ufike mbali na kupata elimu bora na upate timu kubwa kuzichezea Hispania na Duniani katika mpira wa kulipwa". Ameeleza Mhe.Senyamule.

Pamoja na hayo amemtaka akawe balozi mzuri wa Taifa la Tanzania na kuiletea sifa ma heshima na kuweza kufungua milango kwa watoto wengine zaidi wa kitanzania kufika mbali.

Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuzingatia kuwa na malezi bora yenye misingi ya maadili ya Kiitanzania ili kupata vijana waadilifu watakao lisaidia Taifa katika maeneo mbalimbali.

Nae Afisa mahusiano ya kimataifa - Fountain Gate Bw.Dennis Joel amesema binti Mary amekuwa mzuri kwenye masomo yake, kwenye nidhamu na ndo maana amepata fursa ya kwenda nchini Hispania.

"Sisi kama Fountain Gate Academy, kama mtoto anakipaji lakini hana nidhamu, huyo hatokuwa pamoja na sisi, na kuna ambao tumeshawatoa kwasababu hizi kwa maana anakipaji kikubwa lakini hana nidhamu". Amesema Bw.Joel.

Amesema wamekuwa wakiwapeleka wanamichezo wenye vipaji vya mpira wa miguu nchini Hispania ambapo wanafanyiwa majaribio kwa timu kama Barcelona Fc, hivyo muda wowote wakihitajika wanaweza kuitwa.

Pamoja na hayo amesema wanajivunia kwa kupeleka mwanafunzi ambaye ataenda kuwawakilisha vyema hasa kutokana na malezi bora aliyoyapata kupitia taaisisi hiyo.

Kwa upande wake Mary Siyame ambaye amepata fursa hiyo amesema anaend akuiwakilisha vizuri Mkoa wa Dodoma pamoja na nchi yake kwa ujumla hasa kwa kuhakikisha anafanya vizuri kwenye masomo yake pamoja na michezo kupitia kipaji chake cha mpira wa miguu.

Amesema matarajio yake ni kuwa mchezaji mkubwa ambaye anaweza kusimama na kila mtu akaweza kumfahamu Duniani kupitia kipaji chake kwenye mpira wa miguu.

"Kwa kuwa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassani amekuwa mstari wa mbele kwa kuunga mkono juhudi za wanamichezo wanawake nchini, namuhakikishia ninakwenda kufanya vizuri". Amesema binti Mary.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule akimkabidhi zawadi mbalimbali mwanafunzi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule akizungumza katika hafla ya kumuaga binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania).

Afisa mahusiano ya kimataifa - Fountain Gate Bw.Dennis Joel akizungumza katika hafla ya kumuaga binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania).
mwanafunzi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy binti Mary Siyame akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) katiika hafla ya kuagwa kwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania).

Kocha wa Mwafunzi Mary Siyame, wa Taasisi ya Fountain Gate Academy Bw.Aristides Given (kulia) akizungumza katika hafla ya kumuaga binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule akipata picha ya pamoja na mwanafunzi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule akipata picha ya pamoja na mwanafunzi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania), walezi wa binti huyo na viongozi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule akipata picha ya pamoja na mwanafunzi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania), walezi wa binti huyo na viongozi kutoka Taasisi ya Fountain Gate Academy.
Share To:

Post A Comment: