Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Suleiman Msumi kuhakikisha katapila ya kutengeneza barabara iliyokaa bila kutengenezwa inafanya kazi mara moja ili kuondoa kero ya barabara maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Mongella ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya elimu, barabara na maji katika halmashauri hiyo na kubaini barabara ni mbovu zenye zumbi lililo kama unga na kuleta adha kwa wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi waendapo shuleni.

Alisema barabara zilizopo halmashauri hiyo ni mbovu hali inayopelekea wananchi kulalamika huku mitambo iliyopo halmashauri hiyo ikiwa imeota kutu kwa kisingizio cha kupeleka invoice Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) kutengenezwa lakini hadi sasa Temesa wahawajaja kutengeneza katapila hilo.

"Barabara zenu ni za hovyo sana na shuleni pale Mringa,Moivo na hata tulipopita huko barabara ni vumbi tu hivi mnategemea wananchi wanaionaje serikali,yani hamtengenezi barabara hili ligari limekaa hapa mnasema mnatengenea bajeti mwakani huku barabara zenu ni vumbi tu"

Alihoji kwanini barabara ziwe zimeharibika huku mitambo ya kutengeneza barabara ikiwa inaoza tu halafu huko mashuleni yani barabara ni vumbi tu wanafunzi wanafikaje shule..

"Hii ni halmashauri yenye mitambo isiyotembea hizo halmashauri nyingine zinatengaje fedha ilhali hivi ni vitu vinavyotembea kila siku vinahitaji hela vikiharibika sasa kwanini mpango wake uwe mwakani, mipango yenu ipoje siwaelewi halafu na kule shule ya sekondari mnapaua na mbao za mloliondo wakati mmeagizwa mpaue na mbao za mninga yani nyie kwenye miti hakuna wajenzi na hamtendi haki kwa wananchi "

Naye Ded Msumi alisema maji wanapata changamoto kutengeneza katapila hiyo kwasababu Temesa wanawakwamisha kuja kutengeneza katapila hilo na hata wakikumbushiwa barua ya kuja kuliona nakutoa bei ya vifaa hawafiki kwa wakati.

Alisema ashangaa katapila likiwa limepata kutu katika halmashauri hiyo ilhali wananchi wakitaabika na vumbi hivyo ni heri Halmashauri hiyo itengeneze gari hilo huku akiomba wadau wajitokeze kuwapa miti ya aina mbalimbali waweze kuipanda ili waondokane na adha hiyo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Oldosambu katika Halmashauri ya Arusha Dc Wilayani Arumeru Mkoani Arusha Lucas Loshaine wamelalamika ubovu wa barabara katika maeneo yao haswa nyakati za mvua na kiangazi ambapo vumbi limekuwa likiwaadhiri na kupelekea athari katika afya zao na baadhi yao kupelekea kupatwa na vifua vikuu ikiwemo neuomonia kwasababu ya vumbi linalotimka kama unga wa ngano.

Pia waliomba maji yasambazwe ili waondokane na tatizo la maji ya floride yanayowatesa wananchi wa Kata ya Oldonyowasi na Oldonyosambu ambao baadhi yao wamepata shida kwenye viungo vyao vya miili ikiwemo kupata matege sababu ya maji hao

Hata hivyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Auwsa) Injia ,Justine Rujomba alisema maji safi na salama yataanza kufika kwa wananchi Novemba hadi Desemba mwaka huu eneo la Oldonyosambu na Oldonyowasi ili kuondoa tatizo hilo lililowasumbua kwa muda mrefu wananchi hao.


Share To:

Post A Comment: