Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan leo September 18 ameweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya kiwango Cha lami yenye Urefu wa Km 53.2 kutoka Ruangwa-Nanganga ambapo amemtaka Mkandarasi wa ujenzi huo kukumilisha ujenzi kwa Wakati.
Akizungumza na Wananchi wa Kijiji Cha Nandagala ilipofanyika Shughuli hiyo Rais Dkt, Samia amesema lengo la Serikali ni kuunganisha Mkoa wa Lindi kwa Barabara za lami na Barabara za kuunganisha Wilaya.
Pamoja na hayo Rais Dkt, Samia amewahimiza Wananchi wa Lindi kuweka mkazo kwenye kilimo Ili kuinua uchumi wa Taifa na mkulima mmojammoja.
Post A Comment: