Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Arusha Jiji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Wilfred Soilel imetembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Jiji la Arusha ikiwemo Kituo cha Afya cha Levolosi,Shule ya Wasichana ya Arusha Girls,Barabara ya Engosheraton sambamba na eneo Bondeni City inapojengwa stendi ya mabasi ya Mikoani.

Akizungumza katika Ziara hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mhandishi Juma Hamsini amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuacha kushiriki mambo ambayo yanagombanisha chama na Serikali.

"Maneno mengi sana yamesemwa lakini mimi kama Mkurugenzi sijawahi kuulizwa na mwandishi wa habari yeyote hata mkuu wa kituo hichi mganga mfawidhi hajawahi kuniuliza kwa barua wala kwa mdomo wala kwa simu kuhusu mradi huu,Natoa onyo kwa watumishi wangu msemaji wa Halmashauri ya jiji la Arusha ni meya na Mkurugenzi wake."Alisema.

"Hatuwezi tukawa na wasemaji unaposema wewe mwenyezi Mungu amekupa mdomo mmoja maskio mawili maana yake mtumishi usikilize sana uongee kidogo ndio misingi yakiutumishi, lakini ukajisahau mdomo ukageuka kuwa maskio na maskio yakageuka kuwa mdomo utaharibu kila kitu na utatuharibia Chama chetu cha Mapinduzi." Aliongeza 

Hata hivyo Mkurugenzi aliendelea kuongezea kuwa mradi huo fedha zake zilikuja tangu mwaka 2022 fedha na hazikuwa kwaajili ya kituo cha  Afya Levolosi bali ni kwaajili ya kituo cha Afya kaloleni ila kwa busara na hekima za  Baraza la madiwani waliomba baadhi ya fedha zipelekwe levolosi kwaajili ya ujenzi na maelekezo ya Tamisemi kupitia kwa Katibu Mkuu yakiwa yanaelekeza miradi yote ngazi ya chini kutakiwa kufanywa kwa FORCE ACCOUNT.

"Sisi hapa Arusha tunaufinyu wa ardhi ilituweze kutoa huduma bora na majengo mazuri tumekubaliana Halmashauri kwenye vikao vyake halali vya kisheria imekubali kujenga magorofa ya shule pamoja na vituo vya afya na zahanati kwasababu kwa jiji letu hekari moja ni zaidi ya milioni mia moja kupata fidia." Alisema

"Tumeomba kibali Tamisemi tutumie mkandarasi kwasababu gorofa lolote lile lina msingi ya kihandisi ambayo inasimamiwa na CRB na IRB na Institute of Engineering IET,kwahiyo ukienda kinyume huwezi kufika na kama gorofa likiua watu lazima utawajibika,Sisi kama Halmashauri tumewaajiri mafundi wetu tunataka watu waliokizi vigezo na kusajiliwa na IRB na CRB kwaajili ya Labour Force ndiyo wanaweza kufanya ujenzi wa magorofa" Alisema Hamsini


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amesema kuwa Fedha za kujenga kituo cha afya kaloleni zililetwa ila hakukuwa na eneo la kujenga gorofa na kuamua kupeleka fedha hizo katika Kituo cha Afya levolosi .

"Kama kiongozi mwenye dhamana ya wilaya yakusimamia miradi na mambo yote ndani ya Wilaya sikuona sawa kuajiri mkandarasi mwenye bajeti kubwa kuliko kile tulichokuwa nacho na kutafuta mkandarasi mwingine mwenye sifa nakupata majengo yenye ubora na kupata mkandarasi na sasa yuko kazini" Alisema

"Tulisamimisha ujenzi kwa awamu ya kwanza kutokana na ubadhirifu mkubwa wa pesa uliofanyika ambao ulitakiwa kufanyika na ukatufanya kusimamisha ujenzi ilikupata mkandarasi aliyesahihi na tumepata na mpaka sasa tunaendelea na ujenzi." Ameongeza 

Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Timoth Sanga ameipongeza Halmashauri ya jiji la Arusha kwa miradi mizuri na kusimamia vyema utekelezaji wa ilani ya chama na kuupongeza uongozi wote wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya kwakutekeleza vyema yale yote waliyoyanadi katika uchaguzi mkuu kutokana na maendeleo yanayoonekana ni makubwa na kuwahasa viongozi wa mitaa na madiwani kuendelea kutoa elimu kwa wakazi wa jiji la Arusha. 











Share To:

Post A Comment: