Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof . Godius Kahyarara amesema kufutia mabadiliko ya Sheria katika Mashirika ya Reli hapa nchini hivi sasa Makampuni binafsi na mashirika ya reli katika nchi zinazatuzunguka zinaweza kutapa fursa ya kutumia Reli zetu kusafirisha mizigo yao kupitia Tanzania na Sehemu nyingine.

Akizungumza katika kikao cha Ushoroba wa kati kilichohudhuriwa na Makatibu wa kuu wa uchukuzi kutoka Rwanda, Uganda, Burundi, Malawi, Zambia ,Tanzania na DRC,Prof. Kahyarara ameomba nchi hizo kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha miundombinu na kutumia Sekta ya Uchukuzi kama nguzo ya Maendeleo ya Kiuchumi badala ya huduma.


“Hatua kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Mheshimiwa Rais Dr.Samia Samia Suluhu Hassan ni Kuanzisha Usafiri wa kubeba mabehewa kupitia Ziwa Victoria na Tanganyika”. Alisema Prof. Kahyarara.

Kahyarara amesema tayari meli ya kubeba mabehewa kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Port Bell Uganda imekamilika na wakati wowote itaanza kazi.

 “Meli hii itabeba mabehewa ishilini na mbili na inafursa kubwa kuwezesha nchi hasa za Uganda, Sudan ya Kusini na nchi nyingine kutumia reli zao” Aliongezea Kahyarara.


Kwa upande wake katibu mkuu wa uchukuzi toka Burundi Chrisine Niragira ameimiza matumizi ya reli kwa nchi wananchama ,amesema wakitumia Reli kusafirisha Mizigo itasaidia kuokoa Barabara zisiharibike na kutumika kwa muda mrefu. 

‘’Reli inabeba Mzigo mkubwa hivyo nchi wanchama ni muhimu kutumia reli kwani inasaidia kupunguza gharama na pia itasaidia kulinda Barabara zetu amabazo zinajengwa kwa gharama kubwa’’ Alisema Niragira.

Katika Mkutano huo Malawi na Zambia wamejuinga katika Ushoroba huu hivyo kupitia ushoroba huu changamoto nyingi zitazungumzwa na kutafutiwa ufumbuzi ,Mkutano huo wa Makatibu wakuu umefanyia jijini Dar es Salaam.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: