Na Mwandishi wetu Pwani
Naibu Waziri wa uchukuzi Mhe David Kihenzile amepongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini(TPA) za uboreshwaji wa miundombinu ya Bandari za bahari na maziwa.
Mhe Kihenzile ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua bandari ndogo ya bagamoyo, eneo la Mbegani itakapojengwa bandari mpya ya bagamoyo na bandari kavu ya kwala vyote vilivyoko Mkoa wa Pwani tarehe 25 Septemba,2023.
“Nimepata fursa ya kutembelea bandari ndogo ya bagamoyo, kukagua eneo la mbegani itakapojengwa bandari mpya ya Bagamoyo na bandari ya kwala uwekezaji uliofanyika tayari na unaotarajia kufanyika ni mkubwa na utaongeza mapato ya TPA,wananchi , pato la taifa na utasaidia kukuza utalii ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi kimataifa” amesema kihenzile
Mhe Kihenzile amesema ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo yenye eneo la ukubwa wa Hekta 887 unaotarajiwa kuwa na gati 24 ambapo kwa kuanzia imeshatangazwa tenda ya kumpata mkandarasi kwa ujenzi wa Gati tatu zenye urefu wa mita mia tatu kila moja ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo ujenzi wa SGR,ununuzi wa ndege, vichwa vya treni na mabehewa ili kutanua wigo wa kuhudumia mizigo ya ndani na ya nchi jirani zinazotuzunguka ambazo zina mzigo mwingi zaidi.
“Nchi jirani zinazotuzunguka mahitaji yake ya mzigo kwa mwaka ni metric tani mil 40 na uwezo wa bandari zetu kwa sasa ni kuhudumia metric tani mil 8, hivyo ujenzi wa bandari hii utakapokamilika sambamba na maboresho ya bandari zetu zote za bahari, maziwa na bandari kavu za kwala,katosho,ferana ihumwa tutakuwa na uwezo wa kuhudumia mzigo wa metric tani mil 50 kufikia mwaka 2030 hivyo kulihudumia vyema soko la kimataifa” amesisitiza Kihenzile
Akitoa maelezo ya mradi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Nchini Mha Juma Kijavara amesesma eneo la mbegani inapotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Bagamoyo lina ukubwa wa hekali 887 na zoezi linaloendelea sasa ni ukamilishaji wa ulipaji wa fidia na kuwahamisha wananchi ili kupisha mradi na tayari tenda imeshatangazwa ya kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa gati tatu zenye mita mia tatu kila moja.
“zoezi linaloendelea sasa ni ulipaji wa fidia ambapo mpaka sasa shilingi Bil 49 zimeshalipwa kati ya bil 57 zilizofanyiwa tathmini na tenda imeshatangazwa ili kumpata mkandarasi kwa ujenzi wa gati tatu z mita mia tatu na tunaendelea kupokea maombi” amesisitiza Mha Kijavara
Kuhusu uwekezaji bandari kavu, Mha Kijavara amesema uendelezaji wa bandari kavu nchini ni mkakati wa kurahisisha upakiaji na upakuaji wa mizigo bandarini ili kuondoa msongamano na kuongeza ufanisi na kuhudumia mizigo zaidi kwa kuliona hili mamlaka ya Bandai nchini ilianzisha bandari kavu ya kwala yenye hekta 502 ambapo na Nchi jirani zimepewa maeneo, bandari kavu ya Katosho,Fera,Isaka,Iihumwa,Korogwe na Tunduma maongezi yanaendelea ya kupata hekta 500 na maeneo mengine upembuzi unaendelea.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Uchukuzi Mkoa wa Pwani,Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda ameishukuru Wizara ya Uchukuzi na Serikali ya awamu ya sita kwa uwekezaji unaoendelea kufanywa mkoa wa Pwani hususan wilaya ya Bagamoyo unaohusisha ujenzi wa Gati mpya ya mita mia tatu kwenye eneo la bandari ndogo ya bagamoyo na ujenzi wa Bandari mpaya ya bagamoyo kwenye eneo l a Mbegani na Serikali ya Mkoa itatoa ushirikiano wa dhati kipindi chote cha utekelezaji wa miradi hiyo.
Post A Comment: